Kuna umhimu na ulazima wa kuzifufua na kuziboresha shule zetu za vipaji maalum.

nsekwa

JF-Expert Member
Dec 18, 2015
938
1,402
Katika matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa jana, tumeona shule nyingi za Selikali hazijafanya vyema zikiwemo shule zilizovuma kwa miaka mingi hapo nyuma kwa kufanya vizuri. Hapo nyuma ilikuwa adimu sana kuona division zero kwenye shule hizo na ilikuwa kawaida kwa shule hizo kufanya vyema na wakati mwingine kuingia kwenye orodha ya shule bora na kutoa wanafunzi bora kwenye kumi bora. Kwa bahati mbaya sana siku hizi mambo yamebadilika. Shule hizi hazifany vizuri tena. Yawezekana kuna sehemu tulipokosea, yatupasa tujirekebishe na tuzirudishie heshima shule hizi.
Shule hizi zinaendelea kufanya vibaya sababu kubwa ya kwanza ni miundombinu, walimu kutokuwa na ari ya kufundisha, rushwa inayochangia kudahiri wanafunzi wasiokuwa na uwezo kama ilivyo sifa kwa shule hizo, kutokuwepo kwa ufuatiliwaji na uwajibishwaji kwa wakuu wa shule na sababu nyingi sana.

Napenda kuishauri Serikali izifufue upya shule hizi na iangaze hata vijijini ambako kuna watoto wengi sana wenye uwezo na vipaji vyikubwa ambao wangepelekwa shule hizi wangeweza kufanya vyema kabisa kama ilivyo sasa kwenye shule binafsi.
Baadhi ya shule hizo ambazo ningependa Serikali iziangalie tena bila kuchelewa ni:
Ilbolu, Mzumbe, Kibaha, Kilakala, Tabora boys&girls, Ifunda tech, Moshi tech, Tanga school, Msoma tech, Bwiru na nyingine ambazo sijazitaja hapo juu. Ni hakika shule hizi ndizo zilizotoa wataalam wengi katika nchi hii.
Inauma sana pale ninapoona kama vile zimelekezwa!
 
Is like unamlilia marehemu aliyebaki mifupa kaburuni hali ukijua hats kufufuka tu haiwezekani. Matatizo makubwa kwenye elimu yetu ni pale tulipotelekeza wawezeshaji yaani walimu. Ni nani asiejua kuwa GARI nzuri dereva; ama hospital nzuri daktari; ama nchi nzuri raid n.k. serikali ingeboresha kada ya walimu yaani MTU aone proud kuwa Mwalimu hata hzi shule za kata utaziona zitakuwa vipaji maalum. Kinyume cha hapo hayamatokeo yatazidi kuwa worse kuliko hali ilivyo sasa.
 
Tuziboreshe shule za serikali ili watoto wa maskini walingane na watoto wa wakubwa wanaosoma shule hizo. Hilo haliwezekani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…