Kuna ulazima wa kubadilisha namba ya simu baada ya harusi?

my name is my name

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
2,017
2,393
Hivi kuna ulazima wowote wa kubadilisha namba ya simu baada tu ya kuoana? Nyie mnaobadilisha sababu gani inawafanya mbadilishe namba zenu za simu?

1630086268974.png
 
Simu wala haina tatizo. Shida inayokukabili ni tabia yako.

Kama tabia yako itaendelea kuwa ile ile basi hata namba mpya utakayotengeneza itaendelea kuwa ya maovu na mwishowe kuvunjika kwa ndoa ama mauti.

Badili tabia. Usisingizie simu.
 
Simu wala haina tatizo. Shida inayokukabili ni tabia yako.

Kama tabia yako itaendelea kuwa ile ile basi hata namba mpya utakayotengeneza itaendelea kuwa ya maovu na mwishowe kuvunjika kwa ndoa ama mauti.

Badili tabia. Usisingizie simu.
Absolutely true
 
Ushamba tu. Kinachotakiwa kubadilishwa ni tabia na mwenendo wa mtu, sio simu wala makazi .

Kwani simu ndio inaenda kuliwa analiwa au anakula mtu sio simu

Tabia tabia mwenendo maisha mpya.
 
Ni kazi bure tu mana unakuta:

»Namba za mahawara zake wote amezikariri kichwani.
»Pia unakuta mtu huyohuyo aliebadilisha namba bado ana social accounts kama Jamiiforums, Facebook, Instagram, Tweeter na Whatsapps zilezile za zamani.

Hivyo hata ukimbadilishia namba mpya ya simu ni bure tu kikubwa ni kila mmoja kuwa loyal tu.
 
Kubadili namba ya simu ati kisa umeanza maisha ya ndoa ni sawa na kuhama mtaa ukitegemea huko unakokwenda watu watakutreat tofauti coz hawajui tabia zako.. ila haichukuagi muda unakuta hata wenyeji wanaanza kukutreat kama ulivokua treated huko ulikotoka.

Utaigiza kwa siku za mwanzoni ila ukishazoeleka tabia zako halisi utaanza kuzionesha.

Bob Marley aliwahi kuimba..
"You're running and you're and you're running away.
You're running and you're and you're running away.
You're running and you're running,
but you can't run away from yourself"

Everywhere you go, there you are.
 
Kama mtu ni mwaminifu hakuna jambo lolote baya hakuna haja ya kubadilisha namba ya Simu.
 
Mimi na mke wangu namba zetu ni zilezile za zamani wala sijamwambia abadilishe kwasababu namba ya simu kubadilika sio kubadilika kwa tabia.

Lunatic
 
Maoni yangu ni kwamba kama unajiamini na huyo uliyemuoa hakuna haja ya kubadilisha namba, maana ulimchagua kati ya wengi na ulifanya maamuzi bila kurudi nyuma, kubadili namba ya simu hakuwezi kusaidia kitu kama bado haujaamua kwa dhati kuachana na njia zako za zamani.

Mimi binafsi namba yangu ina miaka mingi sijawahi kubadilisha kwani najua uamuzi wa kupokea au kutopokea ni wangu, sasa kwanini nijitese kubadili namba! Nakuhakikishia kuwa hata kama ukibadilisha namba bila kubadili mtizamo wako ni kazi bure, usije kushangaa wewe ndio ukaanza kutafuta namba za michepuko yako wakati ulibadili namba kwa madai kuwa wasikupate.​
 
Sio kwa ndoa tu, ila mtu mwenye tabia ya kubadili badili namba lazima kuna mambo anayaficha

Sijawahi na siji kubadili namba kwa sababu yeyote ile. Labda kuongeza namba.
 
Back
Top Bottom