KUNA TOFAUTI KATI YA MURDER na ASSASSINATION: TUTAMBUE JAMBO HILO KABLA YA KUKOSOA NA KUTETEA.

Jamiitrailer

Member
Oct 20, 2019
39
126
Baada ya rais kutoa hotuba kuwashutumu mabalozi waliohimiza uchunguzi huru na wa haraka,watu wanaoona mambo kwa rangi zake waliona matundu na kasoro katika hotuba ya rais.
Jana,mwenye ID Malcom Lumumba alinyoosha maelezo kwa kina kuelewesha watu ni wapi rais alikosea katika hotuba yake...,na kwa nini mabalozi walikuwa sahihi kusema waliyoyasema.
Lakini leo kuna mtu mwenye ID Jingalao anaandika tena ,akimtaka balozi wa America atoe takwimu za Murder/homicide za America...,takwimu ambazo hata yeye anazipata kiganjani kwake kiurahisi kabisa. Lakini Lengo lake ni kulinganisha hizo takwimu... ,na kwa vile idadi ya mauaji(Murder/ homicide) katika America ni kubwa kuliko Tanzania , hiyo hali imfanye balozi wa America asipate uhalali wa kuongelea au kukosoa mauaji yanayotokea Tanzania.

Kuna tofauti kati ya MURDER/HOMICIDE na ASSASINATION. Assasination ni mauaji ambayo nyuma yake yanafanywa katika msukumo wa kisiasa. Murder/homicide ni mauaji yanayofanywa kwa sababu mbalimbali bila msukumo wa kisiasa.
Kwa maelezo na ushahidi unaotolewa na watu kadhaa ni wazi mauaji yazee Ali Kibao na wanachama kadhaa wa Chadema ni assasination act.
Kitu kibaya zaidi inaonesha ni STATE SPONSORED ASSASINATION.

Ni dalili za state sponsored assasinations ndizo zilizowafanya mabalozi waunge mkono uchunguzi huru.
 
Back
Top Bottom