Kuna shida katika mfumo wa NIDA online?

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
2,098
5,295
Wakuu, toka juzi najaribu kuangalia namba ya nida kwa kuingiza details husika lakini inaniambia taarifa zimekosewa wakati ziko sahihi. Nilikuwa najaribu kupata namba ya nida ya mdogo wangu.

Sasa nikaona isiwe tabu ngoja niangalie kama yangu itakubali maana mimi tayari nina kitambulisho na mara kadhaa nilikuwa naingia kuchukua namba yangu kabla ya kupata hardcopy yake. Ajabu nami ninaambiwa taarifa zimekosea.

Nikahisi huenda shida sio taarifa ni mfumo. Je, wakuu kuna mtu amekumbana na shida hii?
 
Kama una Simcard ya tigo na ulisajilia kwa NIDA yako ni rahisi kupata taarifa zako za NIDA.

Piga menu ya TIGOPESA

1. Chagua namba 6 (jihudumie)
2. Chagua namba 6 tena(huduma kwa wateja)
3. Chagua namba 2 (taarifa zako za usajili)
Utaweka namba yako ya siri na utaona taarifa zako.

Kwenye online system yao kuna ugumu sana kupata hasa ukikosea taarifa ulizojaza awali na wanazozihitaji uzijaze kwasasa.
 
Huu mfimo wao tigo ni mzuri lakini ni mbaya kwa upande mwingine
 
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu washafanya yao wewe tulia tu appeal imeshapita km tangu Juzi na mdogo wako ulikua unajaribu inakwama basi appeal ilikua mwisho jana leo jioni jioni ingiza hizo namba itakubari, hii Nchi michongo mingi usikae kihasara utaumia
mimi nimemaliza chuo muda sana
 
Back
Top Bottom