Kuna sheria inayomtaka mhudumu wa banda la chips kuwa na cheti cha afya kutoka serikalini?

Nyarupala

JF-Expert Member
Jun 2, 2024
320
578
Hello!

Leo katika pita zangu mtaani kwetu makuburi nikamkuta bwana afya wa kata ya makuburi kibangu wanakoromeana na mmiliki wa banda la chips huku mmiliki wa banda hilo akimnyooshea kidole bwana afya kuwa anafanya utapeli kwa kuwa yeye(mwenye banda la chips) ana miaka zaidi ya mitano katika kazi hyo ya kuuza chips na eneo hilohilo na hajawahi kuulizwa kuhusu cheti hicho.

Ubishi uliendelea lakini bwana afya akaondoka pasi na kufanikiwa kumpatia cheti hicho. Lakini cha kushangaza huyu bwana afya tena nikamkuta anadai cheti cha afya kwa muuza duka la mahitaji ya nyumbani.

Hii kitu pia imenishtua sana nkaona niulize kama kuna sheria yoyote inamtaka muuza chips na muuza duka la kawaida kuwa na cheti cha afya?
 
Utaratibu ndio huo mkuu,uwe unauza mama ntilie,chips ,duka la vyakula,matunda etc lazima uwe na cheti cha afya,huwa hawafutiliagi sana ndio mana huwa havizingatiwi,siku wakiwa na njaa ndo wanakuja kukutoa ya kubrashia viatu .
 
Ana maanisha leseni za mamlaka ya chakula na dawa au? Au cheti gani
Cheti cha afya. Kimsingi hiki cheti huwa ni kwaajili ya wahudumu au wafanyakazi wa kampuni au taasisi fulani ili kubainisha kwamba mhudumu aliyekatiwa hicho cheti ana utimamu wa mwili na afya kwa kuthibitishwa na vipimo kutoka kwa daktari.
Sasa swali langu ni,je huyu bwana afya anafuata sheria kwa kuwataka wahudumu wa kuuza chips kuwa na cheti cha afya?
 
Utaratibu ndio huo mkuu,uwe unauza mama ntilie,chips ,duka la vyakula,matunda etc lazima uwe na cheti cha afya,huwa hawafutiliagi sana ndio mana huwa havizingatiwi,siku wakiwa na njaa ndo wanakuja kukutoa ya kubrashia viatu .
Hatari!! Tatizo anafoka sana huyu jamaa na kunakoendea atapigwa makofi
 
Hello!

Leo katika pita zangu mtaani kwetu makuburi nikamkuta bwana afya wa kata ya makuburi kibangu wanakoromeana na mmiliki wa banda la chips huku mmiliki wa banda hilo akimnyooshea kidole bwana afya kuwa anafanya utapeli kwa kuwa yeye(mwenye banda la chips) ana miaka zaidi ya mitano katika kazi hyo ya kuuza chips na eneo hilohilo na hajawahi kuulizwa kuhusu cheti hicho.

Ubishi uliendelea lakini bwana afya akaondoka pasi na kufanikiwa kumpatia cheti hicho. Lakini cha kushangaza huyu bwana afya tena nikamkuta anadai cheti cha afya kwa muuza duka la mahitaji ya nyumbani.

Hii kitu pia imenishtua sana nkaona niulize kama kuna sheria yoyote inamtaka muuza chips na muuza duka la kawaida kuwa na cheti cha afya?
Ndio ipo
 
nadhani wanahangaika na homa ya nyani huko wapeni ushirikiano tu, unakuta muuza kiepe hata minywele ya kwapa hajanyoa na anatoka mijasho kama yotyeee unataka watu waugue? Hahaaaaaaa kidding usafi ni hulka.
 
Ok,sasa bwana afya anatembea na hivyo vyeti kuuzia hao wafanyabiashara,je taaria zilizojazwa kwenye cheti amezitoa wapi? Kwasababu eneo lake la kazi kama bwana afya halina baabara wala vifaa vya kupima magonjwa ya mtu yoyote
 
Samahani mkuu Mimi sio bwana afya mtafute muhusika mjadiliane.
 
Back
Top Bottom