Nimechoka Sana
Member
- May 4, 2024
- 18
- 19
Jiji la Dar es salaam linapitia mgawo mkali wa maji unaoendeshwa kimyakimya huku ukitesa watu wengi.
Mathalani, katika uchunguzi wangu kupitia ndugu zangu wanaoishi maeneo mbalimbali ya jiji hili nimebaini maeneo yote ya Kimara, Ubungo, Mbezi, Gongo la Mboto, Kinyerezi, Tabata, Bonyokwa, Kifuru, Malamba na Stendi ya Magufuli hayapati maji.
Inakuwaje jiji kubwa zaidi la kibiashara nchini, lenye wakazi wengi zaidi kuliko mikoa yote nchini lisiwe na uhakika wa supply ya maji kukidhi uhitaji?
Binafsi nashangaa sana, baada ya Waziri Aweso kufanya ukaguzi wa ghafla na kukuta madudu kwenye baadhi ya ofisi za DAWASA DSM maji yalianza kumiminika kwa wingi. Nini kimejiri baada ya hapo?
Maji yanatoka mara moja kwa wiki, napo yanatoka siku isiyofahamika kiasi kwamba inaweza kutokea ukiwa kazini ukapishana na mgawo huo. Mnategemea tuishi vipi? Aidha, maji haya yanatoka bila pressure ya kutosha kuyapandisha kwenye matanki ili walau uhifadhi kwa matumizi ya baadaye.
Hii nchi kila kitu ni usanii tu. Mvua zimeshaanza kunyesha, mabwawa na mito inayotumika kama vyanzo vya maji ina akiba ya kutosha ya maji, kwanini kunakuwa na mgawo? Na kwanini hamsemi kama kuna shida hii pamoja na kuuambia umma shida iliyopo ili watu wajipange?
Nasikitika sana kuona mambo haya. Maji ni huduma ya muhimu isiyopaswa kupigiwa ramli juu ya upatikanaji wake, na haipaswi kutolewa kama hisani. Kinachosikitisha zaidi ni kutopungua kwa bill zake, utashangaa yametoka mara 4 kwa mwezi lakini bill inafanana na ile ya kipindi yanatoka 24/7.
DAWASA mjitathimini kama bado mnastahili kuaminiwa na watanzania wanaotegemea huduma hii muhimu kwa maisha yao.
Nimechoka Sana kama jina langu lilivyo!
Pia soma: KERO - Dawasa kwanini Hakuna Maji Maeneo ya Kimara, na hamtoi taarifa Yoyote