Kuna mchezo unachezwa Tanesco wa kuyeyusha units ziishe haraka?

toplemon

JF-Expert Member
Mar 26, 2017
4,612
4,716
Kuna mchezo unachezwa Tanesco wa kuyeyusha units ziishe haraka?Au ndo watu wa mitandao wamewapa mbinu zile za kuyeyusha mb zetu nanyie mnazitumia kuyeyushia units za wateja?

Kipindi kila kabla mgao haujaanza huku huwa umeme hakukatiki kabisa na ukikatika unarud kama dk 5 tu sasa tulikua tunanunua umeme wa elfu 90 unakaa karibia miezi 2

Na hapo mafriji yanawaka 24 hrs cha ajabu tokea matengenezo ni migao ianze umeme ulikua unakatwa kwa masaa 12 ndo cha ajab tunanunua umeme wa elfu 90 ule ule unakaa siku 25 pekee

Hili jambo linanishangaza sana, na nilihisi ni sisi wenyewe kumbe ni watanzania wengi hili linatokea
Screenshot_20231231-152134.jpg
Screenshot_20231231-152045.jpg
 
Kwenye hili jambo inabidi watu wajue wako kwenye tariff zipi. Ila matumizi yako ndiyo yanayomaliza umeme.
Hivi umesoma vizuri maelezo ya mtoa post?

Anasema unit alizokuwa anakaa nazo miezi miwili kipindi umeme haukatiki 24hrs sasa hivi anakaa nazo siku 25 haliyakuwa umeme unakatika Hadi saa 12 kwa siku
 
Kwani meter ya umeme inasoma umeme upi? Si, ni ule unaotumia wewe au kuna mwingine. Consumption ya umeme umejaribu kuipima ukajua unatumia nini na nini? Labda una faulty devices na mengine mengi. Hii ya kuibiwa umeme mimi siafiki kabisa
Mimi sija confirm kuwa ni kweli ila nimetoa tu tahadhari kwa kusema kwa Tanzania chochote kinaweza kutokea. Mbona mabando yanaisha bila kutumiwa? Na hili la bando nilihakikisha mwenyewe kwa kufanya experiment yangu ya uhakika kabisa na siyo mara moja. Usiku saa 5 nilinunua bando la masaa 24 nikaweka kwenye simu baada ya kuhakikishia nimezima data. Halafu nikaitoa line. Kesho yake asubuhi saa 12 nakuta sina salio la data.
 
Mjini mipango watu wananunua apartments Dubai na Singapore hukoo
 
Back
Top Bottom