Kuna mambo ya ajabu sana CHADEMA

mtoto wa mchungaji

JF-Expert Member
Oct 24, 2020
279
480
Leo hii mwenyekiti wa maisha wa chama kilichowai kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania ameanza kuzunguka nchi nzima eti kuimiza ujenzi wa ofisi za chama katika wilaya, makata na matawi, wakati ofisi ya makao makuu wanakaa katika kaofisi ka kupanga ka aibu pale Ufipa.
Mambo ya ajabu sana.

Kwa faida ya wasio fahamu, wakati chama kikiwa chama kikuu cha upinzani Tanzania, CHADEMA ilikuwa inapokea rukuzu ya milioni 300 na ushee hivi, hivyo kwa mwaka chama kilikuwa kinapata kama bilioni 3,600,000,000/-, Cha ajabu sasa chama kilikuwa akilipi hata katibu yeyote wa ngazi yeyote zaidi ya katibu mkuu. Kwa jimbo lililokuwa na mwakilishi yaani mbunge ndiyo kulikuwa na ofisi ambayo mbunge ndiyo alikuwa anaingia mkataba na mwenyenyumba, ofisi za matawi na kata ambazo hazikuwa na uwakiishi ni wanachama wenyewe walikuwa wanajichangisha na hawakuwai kupata msaada wowote kutoka katika fedha ya ruzuku.

Viongozi wengi waliandika barua makao makuu hili kuomba fedha kwa ajiri ya pango wakisema tulianzisha sasa kodi imeisha tunaomba msaada, hawakupata. Tena kodi nyingi zilikuwa elfu 20,000 na 30,000 kwa mwezi lakini chama kilichomoa. Walipokuja makandamanda waandamizi walisema mwanachadema anatakiwa kukibeba chama moyoni mwake. Wakati huo tulikuwa tunaita jasho na damu la makamanda kuhakikisha chama kinasonga mbele bila aibu.

Pamoja na kuwa chama kilikuwa kinauziwa fifaa vya uenezi kama bendera na vifaa vingine unaweza jiuliza ruzuku ilikuwa inafanya kazi gani? ila sisi makamanda tulikuwa tunajua tunafanya jasho na damu.

Kwa msio fahamu mnaweza msielewe chama kilikuwaje katika jamii? chama kilipokelewa kwa mikono na mikuu yote, utashangaa kusikia wakati ule bei ya kadi ya mwanachama ilikuwa sh.1500/- tu, lakini wanachama wapya maitaji yalikuwa makubwa mno hadi kadi ilikuwa inauzwa sh. 3000/- hapa inamaana chama kilipendwa na kukubalika kwa 100%.(wakati wa Dr. Slaa)

Mikutano ya Operasheni Sangara na M4C ilishangaza wanachama wachache waliobaatika kujua kuwa chama kilikuwa kinakopeshwa pesa za mikutano hiyo. Yaani hapa inamaana chama na ruzuku ni watu wawili tofauti. Kama kinafanya mikutano kilipe pesa zote iliwemo magari, petrol, posho na vingine. Ilikuwa ajabu sana. Kama kuna kamanda anabisha aje kanisani nipo.

Leo wamekuja na CHADEMA Digitali ya ada ya sh. 2500/- kila mwanachama na wanakadiria kupata milioni 5,000,000/= kwa mwaka sasa kama walikuwa wanapata bilioni 3,600.000,000/= na ushee na ilikuwa analogi sembuse hii milioni 5 ya digitali ndiyo itajenga ofisi? na ikumbukwe kuwa kile kilikuwa kipindi cha Jakaya watu walikuwa na manoti mfukoni, poleni sana makamanda kwa imani kubwa mlioweka kwa CHADEMA ni sawa na huku kanisani kama waumini wangejuwa namna tunavyotumia michango yao ya sadaka wange acha kuleta sadaka. Kwani kunawaumini wengine wanaamini bado kuwa sisi wachungaji tunapeleka pesa kwa Mungu.

Mtoto wa mchungaji.
 
Wakati CHADEMA wanapata milioni 300 kwa mwezi, CCM ilikuwa inapata bilioni ngapi kwa mwezi? CCM imefanya nini mpaka na bado inaendelea kupata na ofisi wanatumia zilezile zilizokuwa za chama kimoja? pia mafuta na posho ziara zote za CCM mafuta yanatoka kwa ma-DED. Mpuuzi wewe, CCM wakitaka kujenga kitu wanachangisha wakuu wa idara na wafanyabiashara kwa nguvu.
 
Maneno yote hayo ya Nini mkuu, kumbuka mda wa kujipendekeza umeisha now tupo awamu sita mkuu pole, na za ukuu wa wilaya napo nasikia haupo mkuu
 
Nadhani dawa ni dawa tu hata kama awamu ya 9. Kupenda kwa breki na maendeleo ni bora zaidi kuliko saccos
Maneno yote hayo ya Nini mkuu, kumbuka mda wa kujipendekeza umeisha now tupo awamu sita mkuu pole, na za ukuu wa wilaya napo nasikia haupo mkuu
 
Ni kweli chadema wamechelewa. Haya yanayofanyika Sasa ilipaswa yawe yamefanyika miaka 8 iliyopita. Lkin siyo mbaya bado muda upo.
 
Hawakuwa na mipango ya ujenzi ofisi. Ila baada ya wanachama wenyewe wa baadhi ya mikoa kuji-organize wenyewe kujenga ofisi, Mbowe ndio kaamua kupita humo humo.

Ndio maana hizo ni nguvu za wanachama, CDM HQ haitoi hata 100 mbovu. Ishtoshe wao wenyewe CHADEMA HQ hawana hata huo mpango wa kujenga ofisi.

Hata huko Arusha na Moshi hakuna michango ya ujenzi wa ofisi inayoendelea.
 
Hivi kwenye swala la ruzuku chama kinachopata ruzuku ni chadema pekee? Mbona vyama vingne hatuoni Mambo ya ruzuku yakiongelewa? Hayo majengo unayoona ya ofici za ccm asilimia kubwa ni majengo ya serikali yaliyopakwa rangi ya chama...Cha ajabu kila mtu anataka kujua matumiz ya ruzuku za chadema tu mbona hatuulizi cuf,ccm na wengine?
 
Hizi nguvu zote unazozitumia kushambulia "madudu"ya Chadema ingekuwa vzr ungezielekeza kwa ccm wenzio na Serikali yao,uwaulize inakuwaje watu wanakula posho millioni 400 kwa siku,na bado wanaachwa kazini!

Bodi ya Tasac inatumia billioni 23!kwa vikao tu Tena ajenda ile ile,na hawajafungwa!

Takukuru inakili ilibambikia watu kesi 147!sasa wamezifuta,na hakuna ofisa aliyefunguliwa mashitaka kwa matumizi mabaya ya madaraka,haya ndio maajabu

Hakuna pesa ya kuajiri walimu,lakini Kuna pesa ya kununua Benz la millioni 400 la Raisi mstaafu.
 
Wakati CHADEMA wanapata milioni 300 kwa mwezi, CCM ilikuwa inapata bilioni ngapi kwa mwezi? CCM imefanya nini mpaka na bado inaendelea kupata na ofisi wanatumia zilezile zilizokuwa za chama kimoja? pia mafuta na posho ziara zote za CCM mafuta yanatoka kwa ma-DED. Mpuuzi wewe, CCM wakitaka kujenga kitu wanachangisha wakuu wa idara na wafanyabiashara kwa nguvu.
Pesa nyingi zilipatikana kwanini chadema walishindwa kujenga Ata makao yao makuu?
 
Bora umesema ukweli, CCM inatumia mabuvu na kuwanyonya wafanyabiashara sababu ya dola mpaka chaguzi wanachangisha wafanyabiashara tena kupita TCCCIA bila aibu
Pesa si mlipewa chadema kwanini hamkujenga mpaka sasa kumekucha ndio mnavuta shuka?
 
Hizi nguvu zote unazozitumia kushambulia "madudu"ya Chadema ingekuwa vzr ungezielekeza kwa ccm wenzio na Serikali yao,uwaulize inakuwaje watu wanakula posho millioni 400 kwa siku,na bado wanaachwa kazini!
Bodi ya Tasac inatumia billioni 23!kwa vikao tu Tena ajenda ile ile,na hawajafungwa!
Takukuru inakili ilibambikia watu kesi 147!sasa wamezifuta,na hakuna ofisa aliyefunguliwa mashitaka kwa matumizi mabaya ya madaraka,haya ndio maajabu,
Hakuna pesa ya kuajiri walimu,lakini Kuna pesa ya kununua Benz la millioni 400 la Raisi mstaafu.
Hilo sio jibu la kwanini chadema Ata makao makuu wameshindwa kujenga
 
Back
Top Bottom