Kuna mama ntilie anauza chakula kizuri. Tatizo liko kwa mwanae, wateja tunapungua

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
May 3, 2022
6,156
10,950
Yaani anapika msosi mtamu sana kana kwamba anaupika akiwa uchi. Tatizo ukienda kwenye mgahawa wake kula chakula, unapakuliwa msosi vizuri tu, tatizo linaanzia kwa mwanae mwenye furushi la makamasi ya njano puani na kitambi kikubwa sana ilihali ni 5 yrs only

Ukiwa unasonsomola msosi, kale katoto kanakusogelea mpaka usoni huku kakikutazama, dakika mbili baadae kanasogeza juso kwenye sahani ya wali, pua yake inalenga usawa wa nyama. Baada ya hapo kanaanza taratibu kuwasha generator, utasikia iiiiiih iiiiih iiiiih aaaaaaaaah aaaaaaah wali! Waliiiiii! Muda huo mama mtu anatazama tu vimbwangwa vya mwanae pasi na kusema chochote kitu. Inafikia hatua watu wanakuona ni mchoyo kumbe sio

Nimeamua kununua dazeni la foili kisha kuweka ndani kwa lengo la kuchukua msosi pale kwake, kisha kuzunguka nyuma ya mgahawa na kukitafuna kwa hasira kali

Ukisema uzunguke na sahani, yule mtoto atakufuatilia kwa nyuma nyuma ilimradi akizangambule. Yaani hata muwe 10, atapita sahani zote

Naiomba serikali ya CCM itusaidie kutatua changamoto hii

Maana mwenyekiti wa mtaa amekaa kimya dhidi ya suala hili ingawa si mara ya kwanza kumfikishia malalamiko
 
Hii biashara ya mama ntilie wengi wana watoto(sio vibaya) ila ni kero kwa wateja, unakuta wafanyakaz wa4 wa mgahawa mmoja wote wana watoto, huo usumbufu wao wakati wa unakula sio kabisa wanatia huruma sana na mama zao hata hawawakanyi.

Mtoto anaombaomba chakula na hela kwa kila mteja na mama hamkemei.

Ishu ya usafi nayo n changamoto kwa wale wanaonyonyesha, wengi ni wachafu. Mwingine mtoto kaenda haja akishamsafisha ajisafishi vizuri.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom