Uchaguzi 2025 Kuna kundi limeibuka linapinga Freeman Mbowe kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Ruwamangi

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
1,257
2,339
Habari wana JF

Kama mtakuwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa mtandaoni kuanzia Insta, x (zamani twitter) facebook na hapa Jamiiforums

Mtagundua kuna kundi kubwa limeibuka kumpinga Mwenyekiti wa chadema Taifa Freeman Mbowe kupitia posits na comments.

Hoja zao kuu ni Mbowe aachie uenyekiti wa chama hicho kikuu cha Upinzani Tanzania

Sababu ni kwamba Mbowe umri wake ni mkubwa!! Maajabu haya!

Wengine wanajaribu kuwagombanisha mbowe na Katibu wake mnyika ati amesusia kazi za ukatibu!

Kimsingi hizo hoja hazina nguvu,
Tujifunze hata kwa wenzetu leo Buden anawania urais kwenye Taifa kubwa kama marekani.

Buden ukimwangalia ni mkubwa sana kwa Mbowe
Lakini kwa marekani sio hoja.

Mbowe bado ni kijana anatufaa kuendelea kuongoza upinzani hapa Tanzania.

Tujiulize wapenda demokrasia hapa nchini ni kwanini watawala hawamtaki Mbowe
Mpaka wanafikia hatua ya kuwarubuni
Watu wamhujumu Mbowe?
Jibu ni moja kamanda Mbowe ni mpinzani halisi.
 
Uhai wa chama kile kwa sasa ni Mbowe.

Japo wapo wengi wanaweza kuwa viongozi ila wamegundua pindi mbowe akitoka tu n rahisi kukisambaratisha.

Yule ni mtu haswa. Nkisema mtu namaanisha kweli

Hilo n kundi la watu wenye nia ya kuona chama kinakufa au kukosa nguvu
 
Habari wana JF

Kama mtakuwa wafuatiliaji wa mambo ya siasa mtandaoni kuanzia Insta, x (zamani twitter) facebook na hapa Jamiiforums....
Pamoja na mapenzi yako makubwa kwa 'Kamanda' Mbowe kitu kimoja tu umezidisha chumvi ni kusema Mbowe ni Kijana. Kama sikosei Mbowe ana miaka 62. Sasa kumuita mtu wa miaka 62 kijana ni mapenzi yaliyopitiliza na ninaweza kusema ni kumkosea heshima.
 
Trust me,huyo mwamba akikiacha chama ndo mwanzo wa chadema kupotea katika medani za siasa,moja ya point ya huyo mwamba kukitunza hicho chama ni kwakuwa muasisi ni baba yake
Fact mkuu.
Yule mtu atakufa na chama chake na wataswma ila wapiiii.

Wanataka chama kukiua
 
Uongozi una miiko,ukiona Mambo hayaendi vizuri,wapishe wengine waonekane sio lazima uwe wewe tuu,ni kupokezana .
 
Iwapo akina Msigwa na wengineo wananunuliwa kirahisi sembuse Mbowe amkabidhi mtu mwingine Chama, CCM watakiua mara moja na deep state yao, bado mifumo yake hailindwi na chochote kama ccm inayolindwa na dola na ni chama dola vilevile. Mbowe watch out. Bora uwaachie urais wagombee siyo uenyekiti.
 
Br Bro kwan we unaishi dunia gani? Chama chake cha republican na wafadhiri wake mpenda vita huyo kimemktaa asigombee kuwa hana uwezo wa kuntest kwenye kinyang'anyiro cha Urais hapo Novemba ikiwa sababu ni umri mkubwa na hilo limeibuka kwenye presidential debate na trump, ambapo alikuwa hajiwezi kabisa hata kuongea mwaka huu fuatilia mambo usitulishe matango pori 🤣
 

Attachments

  • Screenshot_20240701-204858.jpg
    111.7 KB · Views: 3
  • Screenshot_20240701-205102.jpg
    143.6 KB · Views: 2
Hao ni fisiemu. Wanapenetrate migongano. Kwasababu wanajua Mbowe ni mtu madhubuti
 
Free and fair election inayodaiwa kwenye uchaguzi wa serikali za Mtaa na serikali kuu na wabunge uanze kuwa reflected kuanzia ngazi ya chama
 
Hao ni fisiemu. Wanapenetrate migongano. Kwasababu wanajua Mbowe ni mtu madhubuti
Msisingizie ccm katika hili kwanza msigwa alichelewa kutoka wenzie walitoka muda mrefu maana walikuwa waishamshitukia chama alikabidhiwa na akina mzee mtei ndio maana hataki challenge akiamini ni cha kwale unadai democracy nje huku ndani ya chama chako huitaji democracy? Why? Kila anaye furukuta anaambulia zahama mfsno chacha wangwe, zitto, lidu pia hebu km anapendwa aruhusu hiyo nafasi kugombea na wengine aone hule muhuni tu bwana anapewa hela na ccm anakula anakoswa msimamo leo lisu ni wa kusimama juu ya meza kwa ngazi za tofali? Hakuna jukwaa? Anakodi gari? Kweli? 🤣🤣
 
nadhani rekebisha hapo uliposema anatokea republican si sahihi, yeye ni mbeba maono wa democratic.
 
ukimlinganisha mbowe na biden ni kweli mdogo sana kwake lakini si kijana ila pia kama anakidhi matakwa ya kikatiba ya chadema kuhusiana na uongozi ni juu yao wao kufanya maamuzi kumchagua au kutokumchagua, ingawa si vibaya kwake kuachia hatamu ili kupisha mawazo mapya kwenye upinzani wa kweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…