Mjukuu wa Magika
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 537
- 1,056
Nawasalimu kwa jina la jamhuri, nanyi mseme kazi iendelee. Serikali ya mama Samia imejitahidi kuponya madonda na majeraha ya watumishi wengi kwa kuwapandisha madaraja na kuinua kima cha chini cha mshahara na kwa baadhi wamefutwa kabisa makovu kwa kupandishwa mara mbili hasa wale walionyang'anywa madaraja enzi za Magufuli.
Kuna kosa la kiufundi niseme hivyo kwenye annual increment kwani baadhi ya madaraja wamepewa hususani wenye daraja D, pia kwa madaraja fulani wilaya/mikoa mingine wamepewa huku wengine wakiendelea na madaraja yao bila annual increment hususani wenye daraja E na kuendelea pamoja na kutumikia daraja jipya kwa miezi 6 au zaidi.
Hii imekaaje wadau, serikali inamchafua mama anafanya ubaguzi au ni maafisa utumishi wazembe wanachelewa kupeleka taarifa sahihi za watumishi au hazina ndio wanahusika na huu ubaguzi? Wote mnakumbuka kipindi cha JPM walioajiriwa 2016 hadi 2020 mishahara yao ilikuwa midogo wakianza na ngazi ya mshahara D1 hata hivyo hawakuongezewa hata TSH 100 hadi pale walipopandishwa madaraja ukilinganisha na walioajiriwa 2021 na 2022 wao walianza na ngazi ya mshahara D3 hasa upande wa elimu walimu wa masomo ya sayansi. Nawasilisha wakuu karibuni tujadili.
Soma Pia: Annual increment ya 2024/25