KERO Kuna kipande kikubwa cha barabara eneo la Nzega kina mashimo makubwa na hatari kwa usalama wa watumiaji wa Barabara Kuu ya Shinyanga - Singida

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Teko Modise

JF-Expert Member
May 20, 2017
2,270
7,535
Ukitoka mizani ya Tinde kabla ya kufika Nzega hapo katikati kuna kipande kikubwa cha barabara kimeharibika na kutengeneza mashimo makubwa sana kwenye lami.

Hii ni hatari kwa watumiaji wa barabara hii na hasa kwa madereva ambao hawaijui njia hii wanaweza kupata ajali.

Nimepita usiku huu nimeshindwa kuchukua picha.

Wahusika mlifanyie kazi, kodi tunalipa na tozo pia.
 
Mie nikiwa naenda kanda ya ziwa, nikifika zangu Manyoni round about nakula kushoto huyoooo! Naitafuta tabora kwanza kisha tutakutana nzega

Ila nayo kule mwisho mwisho ukiwa unakaribia kuingia tabora ina vilima nyege vingi. Usipokua makini unaeza kuchochora
 
Mkuu unavyosema hapa ndo naanza hiki kipande cha Tinde-Nzega kweli kiko ovyo gari inayumba muda wote. Napita usiku huu.
 
Back
Top Bottom