Kuna kila haja ya kupima afya za wanaogombea uongozi nchini hasa afya ya akili

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
7,396
8,639
Wanabodi,

Watanzania wanajua wanavyotawaliwa na walivyotawaliwa. Kuna mambo yaliyofanywa au kufanywa na baadhi ya viongozi wetu yanatia shaka kuhusu utimamu wao kiafya hasa upstairs.

Haya ni mawazo na maoni yangu. Sijui kama wenzangu mnayaona haya. Na kama mnayaona, mnaonaje ushauri kuwa kuna haja tena kisheria kuweka hitajio la wote wanaogombea uongozi nchi kupimwa afya zao katika nyanja zote.

Hii ni kwa sababu:

Mosi, kuepuka kuwa na viongozi vichaa wanaoweza kuangamiza taifa letu.

Pili, kuepuka kuwa na viongozi wagonjwa watakaotugharimu kifedha hasa wanapochaguliwa wakiwa wagonjwa na kuwa na haki ya kutibiwa maisha yao yote.

Tatu, itaondoa ubabaishaji na ukatili hata mauaji mbali na utekaji.

Nne, itatuwezesha kuwa na viongozi wenye sifa wanaoweza kubadili taifa letu na kulisogeza mbele.

Tano, kwa kuwa na viongozi wenye siha, tutaepuka upotezaji muda ambao unapotea kwenye kujitibia mbali na gharama kifedha kama nilivyoeleza hapo juu.

Sita, tutaokoa fedha na muda ambavyo wangetumia kujishughulikia.

Saba, itasaidia kutoa motisha kwa wanaotaka kuwa viongozi kutunza afya zao vizuri.

Je wanabodi mnasemaje?

1735844517982.png
 

Attachments

  • 1735844821378.png
    1735844821378.png
    736.6 KB · Views: 2
Back
Top Bottom