Kuna kijana mdogo kaniuliza hili swali nikashindwa kabisa kulijibu

popomwitu

Member
Aug 11, 2022
79
198
Naomba msaada wenu wana JF Huyu kijana sijui hili swali kilitoa wapi, ameniuliza mwalimu aliingia darasani akasema "Kama jana ingekuwa kesho, basi leo ingekuwa ni Jumamosi" Mwalimu alizungumza maneno haya siku gani?

Mwenye majibu ya swali hili fikirishi tafadhali ashuke chini hapo, nisije nikaaibika kwa huyu Gen Z.
 
Jibu mbona rahisi tu.

Mwalimu alizungumza hayo maneno siku ya Ijumaa,,Kwa sababu kama jana (Alhamisi) ingekuwa kesho (Jumamosi), basi leo (Ijumaa) ingekuwa Juma Mosi 🤒😎
 
Jibu ni Ijumaa

Kwa nini Ijumaa?

Ikiwa Ijumaa ingekuwa "jana" katika hali ya kufikiria, na "jana" ingekuwa "kesho," basi leo (Ijumaa) ingekuwa ni "kesho" ya "jana" ambayo ni Jumamosi.
 
Jibu ni Ijumaa

Kwa nini Ijumaa?

Ikiwa Ijumaa ingekuwa "jana" katika hali ya kufikiria, na "jana" ingekuwa "kesho," basi leo (Ijumaa) ingekuwa ni "kesho" ya "jana" ambayo ni Jumamosi.
afadhali nimeelewa
 
Kama leo ingekuwa jmosi, kesho inakuwa ni jpili,
Lakini Ki uharisia Jpili ni jana.
Leo ni j3.

Jibu j3.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom