Kuna jamaa yangu kanipa number ya mkewe nimtest kumtongoza kama atakubali

kyagata

JF-Expert Member
Oct 18, 2016
10,294
19,605
Wakuu,hizi ndoa za siku hizi sijui zina tatizo gani.
Kuna huyu jamaa angu amefunga ndoa mwaka jana December na binafsi nilichangia sherehe ya harusi yake.
Sasa bana siku za hivi karibuni namuona jamaa amefululiza kupiga tungi sana so jana nikapata wasaa wa kukaa nae kujua kulikoni mipombe kila kukicha.
Kanifungukia kuwa anahisi mkewe sio muaminifu ktk ndoa yao kwa ushahidi kadha wa kadha.
Akaenda mbali akaniambia mkewe hajui kukataa mwanaume yeyote na kila mwanaume anaemtongoza basi yeye anamkubalia.
Jamaa akaniambia kama siamini nichukue number ya mkewe nijaribu kumpiga sound kisha nimpe mrejesho.
Hapa nipo nawaza hii task niliyopewa na jamaa nikiifanya afu shem akatiki nimtafune au nimpotezee tu?
Naombeni mawazo yenu waheshimiwa.
 
Atakuwa manka au mwaliyamkuja au huko kwa mbeba mikoba.

Mwambie huyo mwenzio akaze roho ajitahidi kula
 
Back
Top Bottom