DOKEZO Kuna harufu ya rushwa kutoka Fedha za Mikopo ya Wanafunzi wa Degree. TAKUKURU chunguzeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Miaka ya nyuma tokea nchi ipate uhuru huu mwaka bajeti ya kutoa mikopo Kwa WANAFUNZI WA degree ilikuwa kubwa sana, ilikuwa TZS bilioni 700+.

Serikali ikakatangaza WANAFUNZI wanaonza degree (fresh students) watapata wanafunzi 75,000 lakini majina mpaka sasa yametoka 73,000 ambayo yamegharimu Sh. Bilioni 200+ sawa na asilimia kama 29 hivi ya bajeti yote huku wanafunzi wengi tukiwa tumekosa mkopo kuliko miaka yote, Ningependa Waziri ahojiwe hizo Sh. Bilioni 500 nyingine zimeenda wapi?

Wanafunzi wengi tuna sifa za kupata mikopo lakini hatujapata mpaka Sasa. Hadi batch zote zimeshatoka na imetoka nafasi ya rufaa Sasa rufaa ina umuhimu gani? Kama pesa zipo ziwagawe kwa wote wanabaki na pesa ili watumie wapi?

System yao pia mbovu inabidi waibadili. MTU akikosa mkopo wamwambie sababu iliyomfanya akose; pia wahudumu wa ofisi za HESLB wengi hawana maadili, wamewekwa ofisini ili wafanye kazi zetu lakini wakipigiwa simu au wakifuatwa wanaleta dharau sana. Ingali na wao pia walisoma kupitia hiyo hiyo mikopo.

Naomba Serikali ichunguze kwenye suala hili. Nilipojaribu kupitia comments kwenye social media zao nikagundua wanafunzi wengi sana waliotokea Diploma hawajapewa mikopo.
 
Wanafunzi mna vichwa vigumu, kama unashidwa kuelewe hii utakuja kuelewe kweli darasani?

Ipo hivi mkuu 700B sio mikopo kwa wanafunzi wa degree peke yako, hiyo ni budget nzima Hapa kuna wanafunzi wa diploma, scholarship za samia, wanafunzi wa continues.

Mwaka wa kwanza budget ni kuwapa mikopa wanafunzi 75,000 kati ya twakimu za bodi mpaka sasa wanafunzi 73,000 wamesha pata mkopo kwenye awamu zote 3, izo nafasi 2,000 zilizo baki ni kuajili ya walio kosa kama akiapili akipata yeye atajumuiswa kwenye hii 2000

Tumia akili kama bodi wangetoa majina yote 75000 kwenye awamu zote 3 alafu watakao appeal budget yao utaleta wewe??
 
Back
Top Bottom