Nyendo
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,330
- 4,692
Kwa tunaopanda daladala halitakuwa suala geni kusikia kondakta wa daladala kaamua kuongeza nauli anayojua yeye, hii ipo sana kwa gari za Mbezi Luisi kwenda Kawe.
Kutoka Mbezi kwenda Kawe kondakta anadai nauli ni 700 na anakuwa na kitabu cha tiketi kilichoandikwa 700 kama uthibitisho, na kutoka Kawe kwenda Mbezi anakata 600 na pia anakuwa na kitabu kilichoandikwa 600 hii maana yake wana vitabu viwili tofauti ambavyo vina nauli 2 tofauti kwa matumizi yao wanayojua.
Leo kuna mtu alilipishwa 700 akaomba arudishiwe 100 yake kwa kuwa anajua nauli ni 600 konda akatoa kitabu cha risiti chenye nauli inayosomeka 700 lakini abiria akasimamia msimamo wake huku akiomba msaada kwa Askari aliyepo barabarani.
Ajabu ni kuwa askari anamuuliza konda kwani nauli ni kiasi gani? Konda akajibu 700. Huku askari akielekea uoande wa dereva na kumuacha abiria na kondakta wakitazamana .
Baadae askari akachukua maamuzi ya kusema ngoja nimrudishie hiyo 100 mimi ili kuua mzozo. Kimsingi askari hakutatua tatizo ila alikimbia majukumu yake aliyotakuwa kufanya kwa wakati huo, kama hakuwa anajua nauli, nadhani alitakiwa kuwasiliana na wapanga nauli ajue kisha atoe maamuzi sahihi.
Je, askari si moja ya watu ambao wanatakiwa kujua gharama za nauli ili kuweka mzani sawa pale inapotokea jambo kama hili? Na kama si wajibu wake nani anatakiwa kusimamia jambo hili ili abiria alipishwe nauli halali?
Pia naona ipo haja ya LATRA wanaopanga nauli kuwa wanatoa kadi maamulu zenye muhuri wao na kila gari la abiria kutakiwa kuibandika mlangoni tofauti na sasa kutumia kuandika kwani makondakta wengi wanadai nauli ziliandikwa zamani.
Kadi hiyo itaonesha hata tarehe ya tamko lenyewe kiwango cha nauli na njia ya gari kuoita hii itafanya makondakta wasiweze kutumia vitabu feki kurasimisha nauli zao za wizi.
Pia Matrafiki waweze kusoma kadi na kujua nauli halisi ili watoe msaada barabarani kwani wao ndio wako barabarani tofauti na LATRA ambao wao hupanga nauli ioa hawakai barabarani.