tang'ana
JF-Expert Member
- Apr 3, 2015
- 11,898
- 15,546
Iko hivi
Kuna mdogo wa ex wangu kamaliza chuo mahali huu ni mwaka wa 3 au 4 kana sikosei.
Basi juzi kati hapo nikakutana na huyu ex wangu akaniambia kama ofisini kwetu au namjua mtu yeyote nimsaidie mdogo wake apate kazi.
Basi bana kuna mdau flani hivi namjua ni hr kwa kampuni hizi za wachina nikampandia akaniambia dogo atume cv,bahati nzuri siku hiyo hiyo wakamfanyia online interview dogo akawa kapata ile nafasi.
Akaambiwa aje Dar kwa ajili ya kusaini mkataba na training ya kama mwezi hivi..dogo kafika dar akaambiwa mshahara ni laki 5, kituo cha kazi kitakua songea ila watamsafirisha wao,watampa allowance ya siku 10 kila siku 55k na pia watamlipia kodi ya nyumba mwaka mzima,akaambiwa nyumba atakayopanga isizidi elfu 80 kwa mwezi.
Cha kushangaza dogo baada ya kuambiwa hivyo kumbe hakuridhika na ule mkataba,wakamuambia ajitafakari mpaka asubuhi ya leo awe amewapa majibu ili mchakato uendelee, so mimi asubuhi hii nimempigia kujua alichoamua cha ajabu ananiambia eti yuko njiani kurudi mkoani kwao kwani mkataba ule hajaupenda akasema yeye alitegemea kituo cha kazi kingekua huko huko mkoani kwao Dodoma coz kuna mambo yake mengine bado anayaweka sawa huko dodoma hivyo kwa sasa hayuko tayari kuishi nje ya mkoa wao.
Aisee nimeshikwa na hasira sio poa,nimempigia dada ake nimemwambia live next time asije akaniambia ujinga wa huyu mdogo wake kwa hiki alichokifanya.
Mkipewa connection zitumieni vizuri wakuu otherwise mnatukatisha tamaa.