Kuna amri 10 za Mungu. Je,ikatokea fursa ya kupendekeza Amri ya 11. Wewe ungependekeza Amri ipi mpya?

greater than

JF-Expert Member
Sep 22, 2018
1,653
3,003
Amri 10 za Mungu
1. Kutosujudia/Amini miungu mingine.
2. Kuitukuza Siku ya Sabato/Sabbath.
3. Usilitaje bure Jina la Mungu.
4.Kuheshimu Baba na Mama
5. Usiibe
6. Usishuhudie uongo
7. Usiue
8. Usidhini
9. Usimtamani mwanamke asiyekuwa wako
10. Usitamani mali isiyokuwa yako

Hizo ndiyo Amri 10 za Mungu,,

Je,ikatokea fursa ya kupendekeza Amri ya 11,Wewe ungependekeza Amri ipi mpya.

Pendekezo langu.
11. Usibet
 
11: Usigongee bia.

12: Ukiona sms ya mwanamke inaanza na 'My nikuambie kitu' zima simu.

13: Usiwaamini Wanasiasa

14: Usiingie choo cha umma

15: Usikanyage Kimboka,Mwananyamala,
Kibo,Wanja wa Fisi na maeneo mengine kama hayo

16: Ogopa Matapeli Wanja wa Shule hauuzwi.
............

Anyway Amri zilianza kumi za msingi ila Israelites walipewa Amri zilizofika 613 na kanuni zake na ole wako ujikwae kwa Moja ni umevunja zote yaani kama leo ni ukipita kibao cha 50 ukapita na 51 Afande akikukamata ukifika mahakamani hakimu anaanza na kosa
1: Uhaini na Kupindua serikali
2: Uhujumu uchumi
3: Ubakaji
4: Uporaji kwa kutumia siraha
Mpaka zote 613 na unapata adhabu ya zote kwa kuvunja kosa Moja
Don't play with Torah
Hua na wazoom Waislamu Wasabato na wanafki wengine wakijifanya wanashika Amri kama wayahudi na kuikataa Neema ya Bwana Yesu ya kuhesabiwa haki kwa Imani na Sio Matendo ya sheria!

Acheni unafki enyi Punda za Herode Sheria hamuiwezi geukieni Neema!😁
Jesus is Lord!
 
Back
Top Bottom