ze kokuyo
JF-Expert Member
- Jan 24, 2014
- 7,417
- 9,603
Mjumbe wa China katika Umoja wa mataifa amesema kwamba sasa ni wakati wa Marekani na Korea kaskazini wenyewe kuelewana kuhusu mpango wa nyuklia na majaribio ya makombora. Amesema si jukumu la China kuiadabisha Korea kaskazini bali ni Marekani na Korea yenyewe kuadabishana. Amesema hayo kama kujibu shutuma za Rais Trump dhidi ya China kwamba haijafanya chochote juu ya Korea kaskazini zaidi ya maneno matupu.
Wakati hayo yakijiri nae Rais Trump amesema kwamba ni wakati sasa wa kushughulika na Korea kaskazini huku Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa bibi Haley akionya kwamba muda wa maongezi juu ya korea kaskazini umekwisha na kwamba sasa ni wakati wa vitendo.Pia amesema kwamba muda umekwisha wa kuitisha vikao vya UNSC kwa ajili ya jambo moja bila mafanikio yoyote na sasa ni muda wa kuchukua hatua baada ya jitihada za kidiplomasia kuelekea kushindwa huku nae pia akiitupia lawama China kwamba haijafanya vya kutosha juu ya suala la Korea kaskazini.
Hayo yakiendelea kufuatia jaribio la juzi la kombora, kamanda wa jeshi la Marekani amesema kwamba Vita kwenye rasi ya Korea itakua ni vita mbaya sana kuwahi kutokea duniani itakayogharimu mamilioni ya watu hasa kwenye mji wa Seoul ambao upo maili 35 toka mpakani na Korea kaskazini. Lakini akliendelea kwa kusema baada ya jitihada zote kushindikana dhidi ya Korea kaskazini hawatakua na namna bali ni kuingia gharama hiyo(vitani) huku akisema kwamba kungoja bomu la nyuklia kutua Seoul itakua ni mbaya lakini kuendelea kusubiri mpaka bomu litakapokua tayari kutua Alaska, Hawaii au New York itakua ni mbaya zaidi.
Korea kaskazini imesema makombora yake yanaweza piga eneo lolote lile ndani ya Marekani.Kilichobaki ni kuendelea kufanya majaribio ya kuweka nyuklia kwenye kichwa cha kombora kwa ajili ya mashambulizi jambo ambalo wataalamu wanasema itachukua muda kidogo (miaka 5-10) kwa Korea kaskazini kufanikisha hilo.Huku wataalamu hao wakisema pia kwamba wanasayansi wa kichina na wale wanasayansi wastaafu wa kirusi wanaisaidia Korea kaskazini kufanikisha hilo.
Huku nako Marekani,Japan na Korea kusini walirusha ndege zao za kivita karibu na mpaka wa Korea kaskazini kama kujibu jaribio la kombora lililofanywa na nchi hiyo.Pia Rais wa Korea kusini ameiomba Marekani kuingeza zaidi mitambo ya kudungua makombora ya THAAD nchini Korea kusini. Pia Marekani nae alijaribu mtambo wake wa THAAD baada ya NK kufyatua kombora la masafa marefu ambao ulidungua kombora kwa ufanisi mkubwa.
Na Japan nao imesema kwamba itaiwekea vikwazo Korea kaskazini.
Huku hayo yote yakiendelea, hapo jana mitambo ya Marekani imegundua uwepo usio wa kawaida wa nyambizi(submarine) inayosadikika kua ni ya Korea kaskazini.