Kumbukumbu za huzuni

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
Tuungane kwa pamoja kusoma waraka wa huzuni.

Kama atarudi tena
akiwa kama mzimu, na kuskia habari
ya yule aliekua akimpenda sana
atauliza kwanza
yuko wapi mtoto wangu?
nini kimetokea kwa mwanangu
nini alifanya?
''maskini mwanangu''
nilimwacha yeye peke yake,
nani alimlinda?
alikuwa na miaka tisa tu
mwaka niliokufa
najua ni vipi alilia sana
huko upwekeni, na shati lililo toboka
likificha kifua chake kidogo
upepo ukimdondosha bila huruma,
au alienda mjini?
'' haujui kuhusu mwanangu?''
amekuwa mrefu?
anafuraha?
anajua kusoma?
ametimiza ndoto zake?
ananikumbuka?
siku ya mwisho ya safari yangu niliyajua haya yote, nilimwambia nitarudi tena

 
Nimegundua kuwa mimi uwezo wangu wa akili ni mdogo sana maana hapa sijaelewa kitu kabisa yaani nimetoka kapa
 
Miss u mama!tangu uliponiacha nkiwa na miaka kumi tu,nimekua mdada now! japo kuna vikwazo napata,matatizoo yanayonirudisha nyuma,upweke,masimango ndani ya nyumba za watu,kuonewa,kuumizwa, sikati tamaa! ipo siku furaha yangu itakuja upya na yote yatabaki story!
 
Pole ndio maisha dada. jikaze tu
 
Tupo pamoja nae, katika furaha tunakumbuka mema yake, tunapokosa msaada tunakumbuka upole wake, kihisia popote ulipo yupo.
 
Pole dada yetu.... mi mtu mingine hairidhiki mpaka ione watu wengine wanasononeka.... Mungu atakuonyesha njia usichoke kumwomba...
 
polee mkuu nusu nidondoshe chozi
 
aggyjay usijali... Umenihuzunisha Sana lakini pambana tu. Mambo yatakaa fresh.
 
I miss my mama too,I was 13ulivoniacha ,nimemis tabasamu lako ,hukukubali nikose kitu,I miss u so much Emma,wangu,kuna saa nahisi nj ndoto huenda ukaamka
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…