Leslie Mbena
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 207
- 677
KUMBUKUMBU;NITAONGEZA MISHAHARA KABLA SIJAONDOKA MADARAKANI-RAIS MAGUFULI.
Matumaini ya wafanyakazi ya kusikia habari njema za kuongezewa mishahara yaliota mbawa baada ya Rais Dk John Magufuli kusema atatekeleza ahadi hiyo kabla ya kumaliza muda wake wa uongozi, hata hivyo, hakuweka bayana ni lini ahadi hiyo itaitekeleza,
Alipoingia Madarakani Mh Rais John Pombe Magufuli alipunguza kodi ya mapato ya mishahara kutoka asilimia 11 ya sasa hadi asilimia 9, kuanzia mwaka wa fedha wa 2016/2017, nikiwa nina mategemeo makubwa waheshimiwa wabunge watapitisha bajeti ya serikali niliyoiwasilisha" Amesema Dkt. Magufuli huku akishangiliwa na maelfu ya wafanyakazi waliojitokeza uwanjani hapo.
Pamoja na uamuzi huo, Rais Magufuli pia amewaahidi wafanyakazi kuwa baada ya kupunguza kodi katika mishahara ya wafanyakazi, serikali yake itafanyia kazi mapendekezo ya kuongeza mishahara.
Wakati matumaini ya kusikia habari njema ya kuongezewa mishahara leo yakiota mbawa, Rais Magufuli ameahidi kuwa katika mwaka wa fedha wa 2019/2020 watumishi 193,166 wa umma watapandishwa vyeo wakiwemo walimu.
“Tangu Novemba 2015 tumewapandisha madaraja au vyeo watumishi 118,989 kwa gharama Sh29.5 bilioni ambapo waalimu ni 75,502 ambao wamelipwa Sh12.3 bilioni na watumishi wasio waalimu ni 43,487 ambao wamelipwa Sh13.2 bilioni,” amesema Rais Magufuli.
Kuhusu madai ya wafanyakazi, amebainisha kuwa wamelipa madai yasiyo ya mishahara yenye thamani Sh291.3 bilioni, mengi ya madai hayo yalikuwepo kwa zaidi ya miaka 10 baada ya kuyaakiki.
Hata hivyo, amemuagiza Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama kuhakikisha bodi ya mishahara inakutana kushughulikia changamoto za wafanyakazi ikiwemo kupanga viwango vya mishahara kulingana na mahitaji ya sekta husika.
#Pumzika kwa amani JPM.