Da'Vinci
JF-Expert Member
- Dec 1, 2016
- 35,772
- 107,381
When I was young and stupid kama ungeniuliza ni mji gani ungependa kutembelea duniani basi ningekuambia mji wa Canton, Canton ni mji ulio kando ya bahari katika nchi ya china lakini kwa sasa hivi uniatwa Guangzhou. Sababu ya mimi kupenda mji huo ni kwakua those time nilikua mpenzi sana wa muvi za kichina hasa zile zinazoExprole masuala ya Shaolin,Budhaism na Kung Fu.
[Mji wa Canton a.k.a Guangzhou]
Canton ni mji uliotoa mashujaa wawili maarufu kama Folk Hero wanaoheshimika sana nchini china ambao ni Wong Fei Hong na Fong Sai Yuk. Moja kati ya waigizaji walionifanya nipapende zaidi alikua Li Lianje (Jet Le) maana kwaigiza hao mashujaa wote katika muvi za Once Upon Time in China 1-3, Last Hero in China kaigiza kama Wong Fei Hong na kaigiza kama Fng Sai yuk kwenye muvi ya Fong Sai Yuk 1-2.
Since I was young at that time kila nilikua nikiona muvi za aina hiyo (zenye mazingira ya kizamani) basi nilikua najua wameigizia Canton. So nikazidi kupenda huo mji. Leo mji huu ni wa tano kwa umaarufu nchini china huko ndio simu za tekno,infinix,itel, zinauzwa kwa visado,debe,mafungu nk. Kama sijakosea wafanyabiashara wengi wa Tz huchukulia vitu mji huo maana upo karibu na bandari.
Wakati wazungu wanaingia nchini china walipapenda zaidi Hong Kong (Rufufu alikua anatamka Hong Kong’a) kutokana na mazingira, hali ya hewa nk. So kule walipajenga vizuri mambo yote mazuri yalikua kule, Dini ya ukristo ilienea zaidi huko. Miaka ya 1960-1970s wachina wengi waliotaka kutimiza ndoto zao za uigizaji walikua wanatamani wafike Hong Kong, ukichunguza utagundua asilimia kubwa ya waigizaji maarufu kutoka china wanatoka Hong Kong mfano Bruce Lee, Donnie Yen, Jack Chen, David Chiang, Gordon Liu, Alxander Lou,Chow Yun-fat, Daniel Wu, Sammo hung, Yuen Biao,Andy Lau, Stephen Chow, Ti Lung nk.
[Moja kati ya muvi bora za zamani inaitwa Five Master of Shaolin: kutoka kushoto yupo Ti Lung, David Chiang, Alexander Fusheng RIP, Lau Kar-Wing na ChinKua-Chun]
Hong Kong ilikua maarufu zaidi upande wa muvi kwasababu kulikua na kampuni kubwa ya utengenezaji na usambazaji wa muvi iliyoitwa Shaw Brother (HK) Studio pia kulikua na madirector wakubwa wawili ambao karibia kila muigizaji wa kipindi hicho kapita mikononi mwao madirector hao ni John Woo na Yuen Woo-Ping. Karibia muvi zote nzuri za kipindi hicho zimetengenezwa na watu hao.
If you’re something of an observer you might have observed and you’re pondering right now that majina mengi ya hao waigizaji mengi yameanza na jina la kizungu na kuishia la kichina mfano Bruce Lee, Jack Chan,John woo, Andy Lau nk. Hear hear sabubu ni kwamba kama nilivyosema HongKong yalikua makazi ya wazungu na ukristo ulikua huko so watoto wengi walipewa majina ya kizungu pengine mtoto alikua anapewa jina la kichina lakini baadae anabadirisha na kujipa la kizungu hivyo mpaka leo hii Wakazi wengi wa hongKong wana majina ya kizungu ila wale wa China Mainland hua wana majina ya kiasili mfano halisi ni Jet Lee. Yeye sio mzawa wa HongKong jina lake halisi ni Li lianje jina lake alipa swagger tu ila hakujipa la kizungu. Salute kwake!
Wu-Tang Birth start with a Bang____Literally
Kwa waliozaliwa miaka ya 2000 inawezekana watashindwa kutambua huyo mtu kwenye picha ila kwa wahenga natumaini wanamtambua. Jina lake halisi anaitwa Gordon Liu, kacheza moja kati ya muvi zangu pendwa na maarufu nchini china/Hong Kong inaitwa 36 Chamber of Shaolin. Ni muvi iliyompa sana umaarufu kipindi hicho kila muvi bomba inatengenezwa na Shaw Brothers Studio kashirikiana na waigizaji wengine kama David Chiang, Ti Lung, nk.
Huyu jamaa kwa sasa ana miaka 72, mwaka 2011 alipata Stroke ya upande wa kulia akawa anatumia kiti kutembelea kutokana na matatizo mbalimbali yaliyokua kwenye familia yake ilibidi ahamie nyumba ya kutunza wazee maana alikua na anapata msongo kutoka kwenye familia zake alioa mara mbili na familia zilikua zinataka mali wakati huo yeye ni mgonjwa.
Alichokifanya mali zake zote alimkabidhi mwanamke mmoja ambae alikua msaidizi na msemaji wake aliyeitwa Eva fung kama mwangalizi, lakini baadae walikorofishana Liu akataka arudishiwe mali zake zote ila Eva akagoma kurudisha mali ambazo hakuchuma yeye ila mzee alikomaa Yule mwanamke akazirudisha akamkabidhi mwanamke mwingine kama muangalizi wa mali zake. Inasemekana mpaka leo hii Gordon liu bado yupo nyumba ya kulea wazee akiwa na stroke…….Turudi nyuma kidogo.
[Gordon Liu katika muvi ya 36 Chamber of Shaolin]
Mwaka 1981 Gordon Liu alitoa muvi moja inayoitwa Shaulin and Wutang, muvi hii ilionyeshwa mpka nchi za ulaya na marekani ikapendwa sana, kupendwa kwa muvi hii kulipelekea maisha ya watu wengi hasa Wamarekani weusi kubadirika.
[Gordon Liu Kipindi hicho]
The Unwritten Policy
Mwanzoni mwa miaka ya 80s na 90s kuliibuka wingi wa madawa ya Cocaine mitaani hasa katika maeneo ya wamarekani weusi wenyewe waliita Crack Cocaine Epidemic mabapo ilipelekea kiwango cha uhalifu na mauji kikawa juu zaidi, ilifikaia hatua kwamba mtoto akizaliwa anakua na option tatu. 1; Auze madawa, 2; Acheze kikapu, 3; Aimbe HipHop na hata mtu ulikua ukiimba hiphop bado unakua affiliated na madawa maana waimbaji wengi walikua na background ya kutumia au kuuza madawa pia wafadhili wao walikua ni Drug Dealers wakubwa kutoka mtaani (Refer tukio la kesi ya Takeshi 69)….Inasemekana (Conspiracy) kwamba CIA kupitia black operation zake walikua wanaingiza madawa USA na kuzisambaza kwenye makazi ya watu weusi ili wao waendelee kubwia unga wakati wazungu wanashika vyeo vya serikali, faida iliyopatikana CIA walitumia kununua siraha.
Kuna chalii mmoja alikua anaitwa Robert Fitzgerald Diggs aliunda group lake lake la Rap akiwa na cousin wake wawili ambao ni Rusel John na Gary Grice japo walikua wanarap ila bado walikua wanajihusisha na kuuza madawa. Mwaka 1992 huyu chalii alipatwa na majanga ya kesi ya mauaji bahati nzuri akakutwa hana hatia, siku alipokutwa hana hatia alijiapiza kwamba hatajihusisha tena na uhuni wa mtaani wala madawa akawekeza nguvu zake zaidi katika kuRap na kuProduce nyimbo. Toka kitambo muvi aliyokua anaipenda zaidi ni muvi ya Gordon Liu iitwayo Shaolin and Wutang, hivyo Robert alivyoamua kujikita zaidi kwenye muziki kundila lake lile alilibadiri na kuliita Wu-Tang Clan. Yeye mwenyewe alijiita RZA (tamka riza/e) album yaooya kwanza aliita Enter the Wu-Tang (36 chambers) ambapo neno Enter alilitoa kwenye muvi ya Enter The Dragon ya Bruce Le, 36 chambers aliitoa kwenye muvi ya 36 chambers of Shaolin ya Gordon Liu.
Kuptia filamu za Gordon Liu Rapper RZA ameweza kua moja ya rapper bora wa muda woote, kasaidia familia yake kuiondoa mtaani, katoa ajira nyingi sana kupitia muziki wake na kulea watoto wake 9. RZA kama sijasahau ni muislam lakini anaheshimu sana imani ya Budhaism na Shaolin kwa ujumla mara nyingi hua ana Meditate.
Motivation ya kufanya kitu sio lazima uipate kupitia vitu vikubwa au watu wakubwa bali hata mambo madogo madogo kama muvi yanaweza kukubadirisha mfumo wa maisha yako. Kuna msemo unasema kwamba “Even a small person can cast a large shadow” kwamba mtu mdogo pia anaweza kutoa kivuli kikubwa…haijalishi wewe ni mdodgo kuwezo au kiumri kiasi gani bado unaweza kufanya kitu kikubwa haijalishi pia hamasa umeipata kwa mtu mkubwa wala mtu mdogo. Kupitia muvi ya Shaolin and Wutang RZA kaweka alama yake katika dunia ya muziki wa HIPHOP pia kafungua record lebel nyingi kama vile Wutang Records, Razor Sharp Record, 36 chambers Record, Wu Music Group, Wu-tang International.
[Robert Fitzgerald Diggs a.k. a RZA mwenyewe]
NB: Sijataka kuwagusia kabisa akina Method Man, GZA, O'l Bastard nk becauseI ’m so Exhausted….let call it a day!
~Da’Vinci.