Kumbuka wewe ni binadamu na utakufa

Billal Saadat

Senior Member
Nov 30, 2022
169
358
Memento Homo. Memento Mori.

Julai 12 mwaka 100 BC katika mji wa Suburra huko Roma ya Kale, alizaliwa mtu aliyekuja kuwa Jenerali wa Jeshi na mtawala mashuhuri wa dola ya Kirumi, Julius Caesar (Kaizari). Kabla ya kuja kuwa mtawala wa Roma, Kaizari alikuwa Jenerali hodari aliyeongoza dola ya kale ya Kirumi katika vita nyingi na kushinda.

Baadhi ya vita hizo ni Vita vya Gallic (maarufu kama Gallic Wars katika historia za vita duniani). Vita vya Gallic ilikuwa ni mapambano ya majeshi ya himaya za Ufaransa, Ubelgiji, Ujerumani na Uswisi dhidi ya dola ya Kirumi. Katika vita hizo zilizodumu kwa miaka nane Warumi chini ya Kaizari walishinda, na kueneza himaya yao Ulaya.

Baada ya kushinda vita vya Gallic, Kaizari akaingia kwenye siasa na kushinda kuwa Mtawala wa Dola ya Kirumi (Consul) akiwa na umri mdogo wa miaka 40. Akawa mashuhuri sana. Akapigana vita dhidi ya mahasimu wake wa kisiasa kama kina Pompei na kushinda, kisha akajitangaza dikteta wa maisha wa Warumi (dictator in perpetuum).

Kaizari anakumbukwa kwa mengi mazuri na mabaya wakati wa utawala wake. Moja ya jambo zuri analokumbukwa nalo ni lile la kuajiri mtumwa (Auriga) kwa kazi maalum.

Ilikuwa hivi, katika kila vita aliyoshinda, akiwa mwanajeshi na baadaye mtawala alipenda sana kufanya maandamano makubwa na farasi kuzunguka Roma kusherehekea. Sherehe hizi zilimfanya ajisikie kama Mungu mtu kwa hiyo akaajiri mtumwa spesho kuketi pembeni yake kwenye kila sherehe na paredi za ushindi kutamka sentensi mbili kwa kurudia rudia muda wote na kwa sauti ambayo ni Kaizari peke yake angesikia. Sentensi hizo ni hizi:

“Memento Homo. Memento Mori”.

Maana yake “Kumbuka wewe ni binadamu. Kumbuka utakufa.”

Kwamba katika ushindi ule mkubwa wa vita na dola ni vyema kukumbuka bado yeye ni binadamu na kwamba yote yatapita. Hivyo yasimjae kichwani na kumvaa kiasi cha kusahau hilo. Funzo kubwa ambalo hata hivyo halikumwingia hata Kaizari mwenyewe kwani baadaye alijitwika ukuu, ukamjaa na kujitangaza dikteta wa maisha wa Warumi, jambo ambalo lilisababisha kuuawa kwake ndani ya ukumbi wa seneti huko Roma akiwa na miaka 55.

Memento Homo. Memento Mori.

59901b2f-f6eb-4ea4-978e-95c05b4f5c43.jpg
 
BC, kumbe hata kabla ya Kristo watu walijua kuna Mungu.
Kumbe hata kabla ya Kristo Ulaya ilikuwepo na watu waliishi na kupigania kutawala.

Memento homo, memento mori
 
Back
Top Bottom