Kumbe Injinia Hersi alisoma Kayumba?

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
16,076
29,753
Akijibu swali la kizushi kutoka kwa Oscar Oscar Wasafi TV, kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡

"Inasemekana ulipokuwa mtoto ulikuwa unaonekana kama una mapenzi na Simba.

Hata mlipokuwa mkicheza chandimu Simba na Yanga wewe ulikuwaga unachagua upande wa Simba, ila sasa hivi umekua Rais wa Yanga. Hebu tuambie hii imekaaje"

Majibu ya Injinia Hersi sasaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Nimekulia jijini Dar es salaam. Nimesoma katikati ya jiji, shule ya Msingi Kidongo Chekundu( AMBAYO NI KAYUMBA/ the emphasis is mine)

Wakati Mimi nasoma Kayumba, wewe ulikuwa kwenu Kaliua. Huwezi kuwa na taarifa zangu za utotoni. Mjini umekuja juzi".

..........

Shule za Kayumba huwaandaa watoto wa kitanzania na uhalisia halisi wa maisha ya kitanzania.

Ewe mzazi, ewe miezi. Acha kuendelea kupunwa.

Huna sababu yoyote ile kuendelea kupoteza hela zako kwa kumlipia mtoto wako pesa nyingi kwenye shule za English Medium ili atakapo maliza chuo aende akawe winga Kariakoo.

Shule za English Medium hazina umuhimu wala upekee wowote kwenye future ya mtoto wako.

Upekee na umuhimu huo umewekwa na wamiliki wa shule hizo ili wakupige hela.

Hizo hela zako unazo poteza ni bora uzitumie kuwanunulia watoto wako assetts halisi kama vile nyumba, mashamba, viwanja, hisa n.k.

Waache wasome Kayumba huku ukiwasimamia kwa ukaribu sana ili wafike sekondari hadi chuo.

Jambo hilo liende sambamba na kuwafundisha biashara na skills za maisha.

Unapolipa mamilioni kwenye shule za English Mediums unacho kifanya ni πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

" kula nyumba, mashamba, viwanja, biashara za watoto wako etc, in the form of an evil spirit who is known as school fees"

Unakuwa kama mtu asiekuwa na akili sawa sawa wala maarifa.

Unamsaidia mmiliki wa shule ya EM kujenga nyumba za watoto wake, kununua magari, mashamba, viwanja n.k vya watoto wake kwa kutumia pesa ambazo ungepaswa kuzitumia kuwajengea watoto wako.

U mjinga kiasi gani wewe. Yani unatoa maji kwenye kisima chako unaenda kuyamwaga kwenye bahari ya mtu mwingine???.

Narudia tena. Shule za English Medium hazina upekee wala umuhimu wowote ule. Upekee na umuhimu huo una exist kwenye mawazo yako wewe mtanzania ambae umekuwa brainwashed na propaganda za Wamiliki wa shule hizo..

Usisahau kwambaπŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Elimu ya msingi ni kwa ajili ya watoto kukua na kusocialize na wenzao Plus kupata just basic knowledge kama vile kujua kusoma na kuandika, KUHESABU, HISABATI, basic geography, basic English Etc. Huhitaji kulipa mamilioni kwa mtoto wako kupata vitu hivyo

πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

MAKING KAYUMBA SCHOOLS GREAT AGAIN πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘‰πŸ‘† MAKAGA CAMPAIGN.
 
Hii tabia ya kupangiana matumizi imeanza lini tena?

Zamani wasichana walikuwa wanachaguliwa waume wa kuoa . Walikuwa hawapewi uhuru wa kuchagua waume wa kuwaoa. Jukumu la kuchagua yupi anafaa kuwa mume wa binti lilikuwa kwa baba wa msichana au wajomba zake au kaka zake wakubwa. Si ajabu hata wewe mama ako mzazi, ni baba ake ( babu yako kizaa mama ako) ndio alimchagulia mume wa kumuoa ( baba yako)

Unajua kwanini walifanya hivyo? Kwa sababu akili ya mwanamke haina uwezo wa kuchagua mwanaume au mume... Women are judges of character. They are generally poor decision makers.

Back to your point. Kuna watu katika jamii yetu , wanapokuwa wanafanya maamuzi yao, wapo kama wanawake katika suala la kufanya maamuzi ya kuchagua mume. They are poor decision makers. They cant make right decisions. Ni jukumu letu kuwaelekeza namna na jinsi ya kufanya maamuzi sahihi.
Nisipokuelekeza mimi leo, kesho utalazimika kufuata maelekezo ya mganga wa kiengeji. Mganga wa kienyeji atakwambia " uende ukaoge njia panda saa 9 usiku"
"Hukwepo wakati nazisaka, Usinipangie Kuspend."

Ngwair - Tupo Juu
 
80 percent ya wahenga wa 40 kwenda juu kayumba was a must, wachache sana made to Arusha school and more
It doesn't change my point. Point ni kwamba alisoma Kayumba...

Wema ni muhenga pia alisoma " a semi international school..

Hamisa Mobetto ni muhenga pia alisoma Kayumba kuanzia vidudu hadi sekondary
 
It doesn't change my point kwamba alisoma Kayumba.

We are not talking about his children mkuu. We are talking about him. Usitoke kwenye mada.
Unatumia sana kiingereza mkuu itakuwa we ni mwanazuoni itoshe kusema uko sawa na umeshinda kuyumba oyee!!
 
Unatumia sana kiingereza mkuu itakuwa we ni mwanazuoni itoshe kusema uko sawa na umeshinda kuyumba oyee!!
Ras Simba aliishia form 2 ila ana miliki maghorofa na vitega uchumi mjini kwa kuwafundisha watu English Course.

Kutumia kiingereza haimaanishi uanazuoni wowote.

Hata TID anaongea kiingereza muda wote ila ni form four failure @ ShebyRoby.
 
LIKUD watu wengi waliozaliwa 1970-1985 wamesoma government schools sio KAYUMBA. Wakati huo hizi shule zilikuwa bora kuliko Private schools bar IST. Mimi nimesoma government school na wakati nasoma tulikuwa na watoto wa Rais Mwinyi, Lowassa, Reg. Mengi na watu wengine wengi tu ambao ingekuwa miaka hii nisingeweza kukaa nao darasa au shule moja. Shule za serikali wakti ule sio sawa na hizi Kayumba sasa hivi.
 
Nimejifunza kitu ndio maana nikasema we mwanazuoni si unaona madini haya mdogo wangu.
 
LIKUD watu wengi waliozaliwa 1970-1985 wamesoma government schools sio KAYUMBA. Wakati huo hizi shule zilikuwa bora kuliko Private schools bar IST. Mimi nimesoma government school na wakati nasoma tulikuwa na watoto wa Rais Mwinyi, Lowassa, Reg. Mengi na watu wengine wengi tu ambao ingekuwa miaka hii nisingeweza kukaa nao darasa au shule moja. Shule za serikali wakti ule sio sawa na hizi Kayumba sasa hivi.
Ngoja jamaa aje ajibu hapa
 
Wewe unachanganya na shule za sekondary za kata ambazo ziliasisiwa na Lowassa kuanzia mwaka 2005.

Shule za msingi ambazo sasa hizi zinaitwa shule za Kayumba ni hizo hizo ambazo tumesoma sisi mkuu.

Jina " Kayumba" lililetwa na lile igizo la " Haki Elimu " la miaka ya 2000 katikati hapo hadi 2010s katikati"

Ila kwa ufupi ndio shule hizo hizo japo nyingi zimeongezwa madarasa ili ziweze ku accommodate idadi ya ongezeko la watoto.

Kwa hoja yako mkuu πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡

Mlimani Primary School ni Kayumba sio Kayumba?

Muhimbili Primary School ni Kayumba sio Kayumba?
 
Hersi kasoma elimu ya msingi miaka 30 iliyopita!!!!

Hicho KIZAZI waliosoma English Medium pengine by estimation hata asilimia 5 sijui kama wanafika...

Kayumba ya miaka ya 90 ambapo darasani tulikuwa hatuzidi 60, leo watoto wanakaa 300, waalim walikuwa walezi leo waalim wanatimiza wajibu.. Miaka hiyo waalim walikuwa wanaumiza kichwa kwanini mnafeli somo lake leo asiyeelewa anaambiwa atajua na wazazi wake...
 
Back
Top Bottom