Kumbe inawezekana mtu akawa kaelimika bila kufaulu mtihani wa darasani kisha utendaji ukaamua kupima kwamba aliefaulu darasani hajaelimika ?

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,923
Mfano kuna kijana anatengeneza vifaa vya umeme kama radio na tv, ana ofisi nzuri tu inayoaminika. akitengeneza tvau radio yako inarudi katika hali yake na unaweza kuendelea kuitumia bila tatizo

Huyu kijana tayari ana elimu ya umeme ila hajasoma akafaulu mtihani wowote unaohusu umeme, kama kasoma basi ni veta. Inamaana kumbe inawezekana tukawa na elimu bila kufaulu mitiani ya elimu ya juu kisha utendaji ukaamua nani ni kaelimika ?

Hapo hapo yupo graduate mwenye degree kutoka UDSM au DIT ambaye amefaulu kwa A za kutosha lakini hana hiyo elimu ya kutengeneza vifaa vya umeme na atahitaji muda tena kuipata elimu.
 
Sasa kwann kupoteza muda kutafuta ufaulu iwapo baada ya kufaulu utahitaji muda kuipata elimu? Si bora twende moja kwa moja kwenye elimu?
 
Mfano kuna kijana anatengeneza laptop na simu, ana ofisi nzuri tu inayoaminika. akitengeneza laptop yako inarudi katika hali yake na unaweza kuendelea kuitumia bila tatizo

Huyu kijana ana elimu ya IT ila hajasoma akafaulu mtihani wowote unaohusu IT. Inamaana kumbe inawezekana tukawa na elimu bila kufaulu mitiani kisha utendaji ukaamua nani ni kaelimika ?

Hapo hapo yupo graduate ambaye amefaulu kwa A za kutosha lakini na hana hiyo elimu ya kutengeneza laptops na atahitaji muda tena kuipata elimu.
Huwezi kuwa master wa kila kitu kila mtu ana fani yake labda useme kama huyo graduate alisoma kutengeneza kompyuta na bado hawezi kutengeneza hapo atakuwa kilaza ila kama hakusoma haina shida.
 
Back
Top Bottom