kule Kenya,Vijana leo wameanzisha maandamano ya kupinga kutekwa kwa kijana mwezao. Tanzania hii haiwezekani tunataka mtu atuandamanie.

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
4,348
11,503
Tanzania narudia kusema Movement za kiuanaharakati hatuziwezi na tunazania mtu mmoja anaweza fanya kwamba kuna mtu anaweza andamana kwa niaba yetu au anaweza paza sauti na sisi tukakaa kutazama jioni kwenye taatofa za habari.

Wakenya wana spirt ya asili ya kupambana na sio kutegemea wakina Raial Odinga na wenzake ambao wana masi binafisi.

Tanzania hii tunaamini kuna mtu labda Mbowe au Lisu au yoyote yule anaweza kufanya hii kazi.

Siasa za kiuharakati ni ngumu sana Tanzania hii ya sasa na sababu kubwa ni nature ya sisi raia na haya maandamano ya vijana Wakenya vijana ni ya ghafla na hayajapangwa na mtu yoyote yule, hayajatangazwa kokote kule.

Saaa sisi tuendelee kuaminishana kwamba kuna mtu anapaswa kuyafanya haya kwa niaba yetu.
Screenshot_20241227_131747_com.facebook.katana.jpg

Hii ni embu leo hii
 
Wakenya linapokuja suala la kupambania maslahi mapana ya Taifa wanaweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja. Na hapa ndipo walipofanikiwa tofauti na sisi tunaoendekeza ubinafsi.

Tunasema kwetu tuna mshikamano kitu ambacho si kweli. Mtu anatekwa mbele ya kadamnasi lakini badala ya watu watoe msaada wao wala hawajali na hapa ndipo wasiojulikana wanapata upenyo wakufanya wanachokitaka kwasababu wanajua hatuna umoja bali ni waoga na tuliojaa hofu.

Kama walau tungekuwa tuna ujasiri hata robo ya wakenya kuna baadhi ya mambo yasingefika hapa yalipofikia sana.

Wenzetu Kenya hawataki sijui tuuende tume italeta majibu wao ni kwenda barabarani hadi wapatiwe majibu yao.
 
View attachment 3186256
Hii ni embu leo hii
yaani mtu alitafute mwenyewe halafu tukalinywe wote?? never anayelitafuta analinywa mwenyewe huo wanafanya wakenya ni uendawazimu sisi hatuna hiyo kitu big NO
 
Wakenya linapokuja suala la kupambania maslahi mapana ya Taifa wanaweka tofauti zao pembeni na kuwa kitu kimoja. Na hapa ndipo walipofanikiwa tofauti na sisi tunaoendekeza ubinafsi.

Tunasema kwetu tuna mshikamano kitu ambacho si kweli. Mtu anatekwa mbele ya kadamnasi lakini badala ya watu watoe msaada wao wala hawajali na hapa ndipo wasiojulikana wanapata upenyo wakufanya wanachokitaka kwasababu wanajua hatuna umoja bali ni waoga na tuliojaa hofu.

Kama walau tungekuwa tuna ujasiri hata robo ya wakenya kuna baadhi ya mambo yasingefika hapa yalipofikia sana.

Wenzetu Kenya hawataki sijui tuuende tume italeta majibu wao ni kwenda barabarani hadi wapatiwe majibu yao.
WAMEFANIKIWA KUFANYAJE YAANI WAMEPATA FAIDA GANI NA HAYO WANAYOYAAMINI NA KUYAFANYA
 
Sasa kama Wanachadema makada wao wanatekwa halafu hawakinukishi kwa nini wabongo wasio na vyama wakinukishe?.

Siasa za Mbowe ndo zimekirudisha nyuma chama hadi kukosa people's power!
 
WAMEFANIKIWA KUFANYAJE YAANI WAMEPATA FAIDA GANI NA HAYO WANAYOYAAMINI NA KUYAFANYA

Haya ni baadhi ya mafanikio ya maandamano nchini Kenya.

1. Hatutaki nyongeza ya mishahara'

Hili huenda ndilo kubwa zaidi ambalo limetokana na shinikizo ya wananchi na hasa kutokana na maandamano ya hivi karibuni .

Ndio hatua muhimu inayoonekana kujibu lalama za wengi nchini humo ambazo zinahusu watu katika nyadhifa kuu serikalini kuwatwika mamilioni ya wananchi mzigo wa kugharamia mishahara yao ya juu na maisha ya kifahari.

Kando na rais William Ruto kulazimika kuufutilia mbali mswada wa fedha uliowasha maandamano hayo,hatua hii ya hivi punde inaingia katika orodha ya 'ushindi' wa waandamanaji.

Ingekuwa ajabu iwapo wabunge,maseneta na rais wangesalia kimya na kuendelea na mambo kama kawaida iwapo notisi hiyo ya SRC ya kuwaongeza maafisa wakuu serikalini mishahara ingetekelezwa .

Viongozi wengi kwa kauli moja waliikemea hatua hiyo ya SRC kutoa notisi ya nyongeza ya mishahara wakati huu hasa baada ya maandamano ya wanancha na wakikariri msimamo wa rais Ruto kwamba uchumi kwa wakati huu hauna nguvu kuweza kubeba mzigo wa nyongeza hiyo.

Kenya kwa sasa inatumia zaidi ya shilingi trilioni moja kuwalipa wafanyakazi wa umma, na kuna ongezeko la shilingi bilioni 29 la fedha zinazolipwa kama mishahara kwa watumishi wa umma licha ya tume ya mishahara kuzuia nyongeza ya hivi punde. .

2. Michango ya Harambee
Iwapo kuna kichocheo cha wazi kwa maandamano ya vijana ,ni hatua ya wanasiasa na watumishi wa serikali walio karibu na viongozi wakuu wa nchi kuonekana hadharani wakibeba na kutoa vitita vya pesa katika michango -mara nyingi katika makanisa .

Maonesho hayo ya utajiri yameashiria kutojali kwa upande wa maafisa wa serikali wanaohusika na michango hiyo.

Katika nchi ambayo wengi wana matatizo ya kichumi,mabunda ya noti machoni mwa watu ambao wanatatizika kupata hata mlo mmoja kwa siku ni chanzo cha hamaki ambayo imetokota kwa muda .

Mlipuko wa hamaki hizo ulionekana katika maandamano ya vijana wa Gen Z.

Rais William Ruto aliahidi kwamba atachukua hatua kuhusu hilo wakati alipoashiria kwamba labda wakati umewadia kwa harambee kupigwa marufuku hasa kwa maafisa wa umma .

Michango kama hiyo inashukiwa kuchochea ufisadi na inahofiwa huenda fedha za umma ndizo hutolewa katika hafla hizo.

Baadhi ya viongozi pia hawajatuliza mambo kwa kupiga picha wakiwa katika magari ya kifahari, ziara za nje ya nchi na wakistarehe katika maeneo mbalimbali ya burudani .

Iwapo maandamano ya vijana yataleta kikomo kwa 'show' hizi kubwa za ni yupi aliye na hela nyingi ,gari kubwa au jumba bora la kifahari ,basi yatakuwa yamepata ufanisi wa kuleta aina fulani ya nidhamu.

3. Mwisho wa siasa makanisani?
Iwapo kuna ushirikiano ambao unaonekana kuwaghadhabisha wengi nchini Kenya ,ni ule kati ya viongozi wa kisiasa na wa kidini .

Vijana waliokuwa wakiandamana wiki mbili zilizopita walikemea vikali ushirikiano huo ambapo kwa kawaida wanasiasa nchini Kenya wamekuwa na nafasi ya wazi ya kutumia kumbi za kidini na hasa makanisa kupiga siasa,kurushiana cheche za maneno na kila aina ya matamshi ambayo hayafai kutolewa kanisani.

Kupitia kauli yao ya #Occupychurches walianza kuwazuia wanasiasa dhidi ya kuwahutubia waumini makanisani.

Ujumbe wa vijana unaonekana ulichukuliwa kwa uzito na viongozi wengi wa makanisa ambao sasa wamewapa notisi wanasiasa kwamba hali haitakuwa kama ya kawaida .

Hili ni jambo ambalo litachukuliwa kama ushindi kwa waandamanaji wa Gen Z kwani ulikuwa mtindo wa kawaida kila Jumapili kuchanganya dozi ya injili na ile ya siasa .

Kwa muda mrefu hatua hiyo iliwakera wengi na sauti za pingamizi zimekuwa wazi katika maandamano hayo .

Viongozi wa kidini pia wameshtumiwa kwa kusalia kimya wakati serikali ilipokuwa ikipendekeza sheria kali za ushuru ambazo zilionekana kuwaacha wengi katika hali mbaya kiuchumi katika mazingira ambayo tayari gharama ya maisha imewalemea wengi .

Iwapo viongozi wa kidini watataka kusalia na hadhi ya kuheshimika katika jamii,watalazimika kuchukua hatua za wazi kujitenganisha na ushirikiano wao na wanasiasa na kupaza sauti zao kupinga kinachotafsiriwa mara nyingi kama uovu wa watawala .

4. Uwajibikaji wa kisiasa
Iwapo kuna ushindi mkubwa ambao utaletwa na hatua ya vijana kwenda barabarani ,basi kuleta uwajibikaji kwa viongozi waliochaguliwa ndio utakaokuwa ushindi muhimu sana .

Athari za mwamko huu mpya zimeanza kuonekana.

Pingamizi ya wananchi dhidi ya mswada wa fedha ilikuwa wazi.

Wananchi walituma jumbe kwa wabunge wao,walifoka mitandaoni na kupiga kila aina ya kelele kusikika ,lakini viongozi wa kisiasa walifumbia macho malalamishi hayo na kupitisha mswada huo .

Wabunge wengi waliopiga kura ya 'Ndiyo' sasa watakuwa na kazi ya kukutana na wapiga kura.

Baadhi yao wameanza kuomba msamaha kwa wapiga kura katika maeneo bunge yao .

Iwapo watasamehewa ama adhabu ya wapiga kura ipo njiani ,ni jambo litakalosuburiwa hadi uchaguzi wa mwaka wa 2027.

Tayari chama cha upinzani cha ODM kimesema kimeanzisha mchakato wa kuwarejesha nyumbani wabunge wake sita ambao walipiga kura ya kuunga mkono mswada huo wa fedha .

Makali ya ufanisi wa maandamano kuhusu kuwaajibisha viongozi wa kisiasa kwa kweli yatakuwa wazi wakati wa uchaguzi.

Iwapo kutakuwa na athari ya kampeni ya kuwataka viongozi kuwatumikia ifaavyo wananchi ,majibu yatakuwa wazi kupitia kura kwa sababu kwa muda mrefu wanasiasa wamekuwa wakitegemea sana usahaulivu wa wapiga kura .

Wakati huu ni wazi kwamba wanakabiliana na kizazi kisichosahau na chenye ushahidi unaowachwa kote mitandaoni kuhusu 'madhila' wanayotendewa na waakilishi wao.

Swali litakuwa iwapo 'ulimama na sisi' wakati wa matatizo yetu au ulikwenda kuyashughulikia maslahi yako binafsi.

5. Kubana matumizi ya fedha za umma
Daalili nzuri ya uwajibikaji katika matumizi ya fedha za umma ilionekana pale rais William Ruto aliposisitiza kwamba sasa kuna haja ya dharura ya Kenya kubana matumzi ya fedha za umma .

Kwanza ameashiria kwamba huenda afisi zisizo za kikatiba kama ile ya Mke wa rais na mke wa naibu wa rais zikaondolewa na mgao wa bajeti kwa afisi hizo kuelekezwa kwa matumizi mengine .

Hatua hiyo haingechukuliwa endapo vijana wa kizazi Gen Z hawangeandamana na kuzua maswali muhimu sana kuhusu matumizi ya fedha zinazolipwa kupitia kodi na wananchi .

Ingawa rais Ruto ameelezea kwa kina athari za kukataliwa kwa mswada wa fedha ikiwemo serikali kupunguza migao kwa sekta muhimu za umma,serikali za kaunti ,kukosa kuwaajiri walimu na madkatari zaidi ,amekariri pia umuhimu mkubwa uliopo wa nchi kuangalia upya jinsi inavyotumia fedha zake zinazokusanywa kama mapato ya ndani .

Alisema ni wakati mwafaka pia kuangalia kiwango cha mishahara ya maafisa wakuu wa serikali na akaeleza kuwa yuko tayari kupunguziwa mshahara katika jitihada za kuurahisisha mzigo kwa mlipa ushuru.

Kenya ingali inazongwa na madeni makubwa na itahitaji kuangalia kwa umakini matumizi yake ya fedha ili kuafikia malengo yake ya kimaendeleo .

Wataalam wa masuala ya kiuchumi wameafiki kwamba kiasi kikubwa sana cha fedha za umma hupotea kupitiia utumizi mbaya,ufujaji na ufisadi.

Mianya hii mikubwa ndio donda sugu katika utawala wowote na huenda suluhisho la kudumu lisipatikane endapo viongozi wa nchi hawataonyesha nia ya kupambana na maovu hayo kwanza kabla ya kusonga mbele .

Malalamishi ya vijana walioandamana yameifanya nchi kuanza kuyazungumzia mambo hayo .Ushahidi wa mazungumzo haya muhimu ulikuwepo siku ya Jumatano katika bunge la seneti ambapo maseneta walifungua nyoyo kuzungumzia yote haya na yanayohitaji kufanyika ili Kenya kuitumia fursa hii kama funzo na kuweza kujiweka katika mkondo ufaao wa historia .

Iwapo kuna zawadi ambayo vijana wameipa Kenya kupitia maandamano yao ,ni fursa ya kuyazungumza kwa uwazi mambo haya na kuyatafutia ufumbuzi .

chanzo: BBCSwahili

Kweli kabisa ni nchi ya ajabu.

Walimtegemea Julius Nyerere

Wanamtegemea Freeman Mbowe

Wanamtegemea Mama

Wananategemea hisani ya chama dola tawala kongwe CCM

Wanamtegemea Mola

Tanzania ni nchi ya kumkabidhi mtu mmoja awabebe, na sasa wanamtegemea Tundu Lissu

Watanzania kwa makundi madogo kujiweka pamoja hawawezi huwa wanamtumainia mtu mmoja au chama fulani kikicho kikundi cha watu wachache wawe wanawasemea shida, changamoto, katiba, uhuru na haki.

Kujitokeza kundi kubwa la umma nje ya hayo makundi hapo juu watanzania hawawezi pamoja na wingi wao kama umma mpana, hata kutengeneza movement nje ya CHADEMA, CCM, TLS, BAKWATA, CCT n.k hawawezi
 
Tanzania narudia kusema Movement za kiuanaharakati hatuziwezi na tunazania mtu mmoja anaweza fanya kwamba kuna mtu anaweza andamana kwa niaba yetu au anaweza paza sauti na sisi tukakaa kutazama jioni kwenye taatofa za habari.

Wakenya wana spirt ya asili ya kupambana na sio kutegemea wakina Raial Odinga na wenzake ambao wana masi binafisi.

Tanzania hii tunaamini kuna mtu labda Mbowe au Lisu au yoyote yule anaweza kufanya hii kazi.

Siasa za kiuharakati ni ngumu sana Tanzania hii ya sasa na sababu kubwa ni nature ya sisi raia na haya maandamano ya vijana Wakenya vijana ni ya ghafla na hayajapangwa na mtu yoyote yule, hayajatangazwa kokote kule.

Saaa sisi tuendelee kuaminishana kwamba kuna mtu anapaswa kuyafanya haya kwa niaba yetu.
View attachment 3186256
Hii ni embu leo hii
Tangulia tukufuate
 
Sasa kama Wanachadema makada wao wanatekwa halafu hawakinukishi kwa nini wabongo wasio na vyama wakinukishe?.

Siasa za Mbowe ndo zimekirudisha nyuma chama hadi kukosa people's power!

Hapa tunaongelea taifa na siyo mambo ya vyama .. Maandamano huko Kenya yalipoanza wala hawakujali huyu sijui ni ODM ya Raila au UDA ya Rutto. Wakenya waliweka tofauti za kidini, kikabila, elimu hawakujali mimi ni msomi au la wote waliingia barabarani.
 
Kabisa huku tunaamini katika mtu
 
Mtanzania anayesihukuru ATM kwa kumpa fedha zake mwenyewe ni tofauti sana na Mkenya.
 
Back
Top Bottom