Habari zenu wana jamii,
Wakati naendelea kulisukuma gurudumu la maendelea nikaona niwaze kwa sauti kuhusu hii tabia ya kula chabo. Kimsingi, kula chabo ni tabia ya kimbea iliyovuka mipaka, yaani mtu anakua ameshikwa na ashki majununi kwa kiwango cha kupenda kutazama wenzake wakiwa wanafanya ngono au kitu kingine chochote kwa usiri bila ridhaa ya wafanyaji. Mla chabo akipata ridhaa ya wafanyaji basi anakua matazamaji (spectator) na dhana ya chabo inakufa. Chabo imekua imezoeleka kufanywa physically yaani kwa uwepo wa mla chapo katika eneo la tukio. Kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia, chabo imekua hi tech, yaani inaweza kuliwa kwa kutumia vifaa vya kieletroniki bila ya mla chabo kuwepo eneo la tukio.
Kwa muktadha huu basi, chabo inaingilia haki za faragha za waliwa chabo na inaweza kuchafua sifa njema ya waliwa chabo kama rekodi ya chabo ziliyofanywa kielectroniki zikisambazwa kwa jamii bila idhini ya waliwa chabo. Hivyo basi, ni rai yangu kwamba wale wote wenye tabia au mazoea mabaya ya kula chabo waache mara moja, kwani chabo ni adui wa haki za waliwa chabo.
Naomba kuwasilisha.