tamuuuuu
JF-Expert Member
- Mar 10, 2014
- 20,876
- 27,205
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro.Mkenda kuna shida kubwa sana sana ya watoto kukosewa usajili wa majina yao sahihi ya awali, kati na ubini. Hili jambo limekuwa ni kubwa na tatizo sana kwa sasa kila kona ya Tanzania. Kwa mfano,
John -Joni
Peter-Pita
Rehema-Rehem
Na mengine kukosewa kabisa jina lote.
Na shida hii inaanzia darasa la nne ambapo ndiyo hatua ya awali ya mtoto kuanza kufanya mitihani ya taifa. Hili limetokana na kukosekana kwa umakini wa walimu husika pindi wanapowasajili watoto. Shida ikitokea katika hatua hii mtoto atabaki na majina yasiyo sahihi milele, na mkanganyiko katika vyeti vyake.
Mfano, cheti cha kuzaliwa kuwa tofauti na vveti vya taaluma.
OMBI:
1. Tunaomba msaada yawepo marekebisho kabla ya vyeti vya darasa la saba kutoka.
2. Uwepo utaratibu wa watoto kusajiliwa kwa majina yao sahihi wanapoanza kidato cha kwanza.
Tunaumia sana kuona watoto majina yao yameharibiwa kabisa kabisa na hayaeleweki ni vitu gani?
Lakini pia huko kwenye shule umakini wa usajili uwe mkubwa,kuna uzembe upo katika hili.