Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,204
- 26,195
Jumapili saanane usiku na jumatatu ya Pasaka haikuwa njema.
Umeme ulikatika karibia nchi nzima.
Chanzo cha tatizo kilikuwa kujizima mitambo huko Kidatu
Tumeelezwa na TANESCO kuwa , kujizima huko kunatokana na maji "kuzidi" na mitambo kujizima.
Maelezo hayo kimsingi hayana maana kabisa kihandisi.
Maana kwenye nyumba unapata maji kwenye mabomba na kuna mifareji ya kuondoa maji, hivyo " kuzidi" ni suala ambalo halipo, pengine itokee mifereji ya kuondoa maji izibe, au koki za kuingiza maji nyumbani zifeli.
Kwa Kidatu mitambo " kuzidiwa maji" hapa TANESCO hawatuelezi ukweli.
Mimi nimetembelea mtambo wa Kidatu siku nyingi kidogo. Maji yanayo ingizwa mtamboni yanatoka kwenye bwawa, mfereji unaitwa Headrace Tunnel ambao una kilometa 11.
Maji yakifika juu ya mitambo minne kwa mabomba makubwa yanayoitwa Penstocks, maji yanateremshwa kwa presha kubwa sana ya nikikumbuka vizuri ni mita 70 au 100.
Hivyo msukumo wa maji kuendesha Turbines zote 4 huwa na mgandamizo mkubwa sana.
Baada ya hapo maji yakisha sukuma Turbines, hutokea kwa mfereji uitwao Tailrace Tunnel na kurudi mtoni pale Mkamba Kidatu.
Sasa system ya maji na mgandamizo wake, maji muda wote yana sehemu ya kutokea.
TANESCO watupe sababu za kimsingi, maji KUZIDI kwenye mitambo does not make sense.
TANESCO semeni kuwa kuna bomba la Penstock au mfumo wa maji yanayolisha Turbines umepasuka, au kwa lugha rahisi, koki ya kulisha mitambo imeharibika, hivyo maji kutoka na kumwagika kwenye system yake ya mgandamizo.
Na hilo litakuwa ni suala la Maintainance ambayo haijafanyika.
Na huo ni uzembe.
Hatufanyi kazi TANESCO lakini logic ya maeleza waliyotoa TANESCO inakataa kueleweka.
Na kwa bahati sisi wengine si wakulima au wanasiasa wasiojua hiyo mifumo.