Kukaa na wakwe mijini inatesa sana, wawe wepesi kusoma alama za nyakati

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Wakati tunajiandaa kuingia kwenye weekend yetu "dume", embu tutafakari kidogo ugumu wa maisha hasa ndani ya jiji la Dsm, jiji la Makonda Paul.

Kuna kila sababu ya kukubali tu kwamba maisha ni magumu, tight haswa, binadamu wanavuja jasho mwili mzima wakihaha kupokonyana mkate wa kila siku. Idadi inayokadiriwa kuwa Million 5 ya wakazi wa Dsm wanapishana kila kukicha,si asubuhi, si mchana, si jioni, si usiku kucha...wakisaka tonge hilohilo moja. Fursa ndani ya Dsm ni very limited, chache kwelikweli.

Unakuta mtu ana familia, hajasoma, ana ndugu (wazazi,wakwe) nyumbani na hali hii, anapumua kwa taabu.

Mbaya zaidi wakwe nao hukaa muda mrefu sana mijini, hawanaga papara ya kurudi kijijini mapema. Anaamka, anapiga chai, mchana kama kawa huku akifuatilia vimichezo kwenye runinga, taaratibu bila shida. Inatesa mno.

Kwa hali hii, kwakweli ikifika mpk June 2017 bado umebanana ndani ya Dsm, wewe ni komandoo, dume na umeshakubali kwenda na kasi ya sasa.

HAPA KAZI TU.
 
Sasa unatuambia sisi tufanyeje? Cha kukusaidia tu nipe namba zao niwapigie niwaambie waondoke
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…