DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 310
- 279
Wanabodi,
Kupokea na kuuza nje bidhaa mbalimbali ni jambo la muhimu na la kawaida katika nchi yoyote. Kulingana na uhitaji wa bidhaa mbali mbali au mahusiano kati ya nchi moja na zingine, bidhaa huingizwa kukidhi mahitaji haya au huuzwa nje ya nchi kuiingizia serikali na makampuni husika kipato.
Uwezo nchi kubobea katika kuuza bidhaa mbalimbali kwanza kabisa, hutegemea uzalishaji wa bidhaa hizo katika viwango vinavyo kubalika. Hii ina maanisha kwamba uzalisha katika sekta tofauti tofauti ukiwa juu basi nchi itaweza kuchangia katika kuwawezesha wananchi wake kukidhi mahitaji yao na ikiwezekana kupata sarafu ngeni kwa kuuza bidhaa hizi katika nchi zingine.
Katika ukuaji wa uchumi wowote, uzalishaji wa bidhaa katika sekta mbalimbali ni chachu katika kufikia malengo ya muda mrefu ya kiuchumi.
Sera ya serikali ya viwanda ni sera ambayo inaweza kutusaidia kufikia malengo yetu kiuchumi kama Tanzania kwa kuwa nchi ambayo sio tegemezi.
Sina takwimu za kutosha kuhusu hili lakini kama tunapokea bidhaa karibia zote tunazohitaji kutoka nchi zingine basi mifumo tuliyonayo sio dhabiti katika kuchochea maendeleo yenye tija. Vile vile mwenendo huu unadhihirisha kwamba kuna mianya mikubwa kwenye masoko ya bidhaa mbalimbali ambayo yakipata muwekezaji anayeweza kuzalisha bidhaa hizi nchini basi matokeo kwa muwekezaji huyo na kwa watanzania yatakuwa chanya.
Katika kuongeza uzalishaji, sera ya serikali ya viwanda inaweza ikaleta mabadiliko ikiwa serikali haita tegemea wawekezaji kutoka nje. Yaani serikali yenyewe ikifanya tafiti za kutosha na kukusanya mtaji wa kutosha inaweza ikawa muwekezaji namba moja na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika kuziba pengo lililojazwa na bidhaa nyingi kutoka nje.
Kwenye hili, ni muhimu kukamata masoko mbalimbali ya bidhaa nchini Tanzania ikiwa mwanzo wa kuweza kuuza bidhaa hizi nchini na nje ya nchi.
Jambo hili linahitaji ujasiri na nguvu kazi kubwa ila maamuzi magumu kama haya na yenye malengo ya muda mrefu yanaweza yakawa njia pekee itakayo tuwezesha kufikia malengo mazuri.
Ni muhimu pia kuelewa kwamba tunapopeleka bidhaa sokoni, ushindani ni kitu cha kawaida na kwasababu hiyo mbinu ambayo inaweza kutumika ni kuongezea kodi bidhaa zinazotoka nje au kuwa na uchaguzi wa kina katika sekta ambazo tunahitaji bidhaa kutoka nje. Kwa sasa, hatuna njia yoyote ya hoja zetu kuhusu kupokea bidhaa mbalimbali kusikilizwa kwa sababu hatuna jeuri hiyo.
Sisi ni tegemezi na kwasababu hiyo, tutatumiwa hivyo hivyo.
Mapendekezo haya ni magumu lakini ndiyo tunayohitaji kubadilisha mwendendo wa serikali kwa ujumla na maisha wa watanzania. Tuelewe kwamba hii ndiyo safari itakayo tuwezesha kujifunza teknolojia mbalimbali zitakazo tuwezesha kwenye uzalishaji, kuwa uhuru kiuhalisia na kujitegemea
Jummah Kareem…