Kujitambua ndio njia ya kwanza ya mafanikio

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
32,189
75,623
Nivigumu sana kukuta mtu asiejitambua kukuta kafanikiwa!.. ila nivyepesi sana kukuta mtu anaejitambua kafanikiwa.
kwenye jamii yetu nimeshashuudia mtu ana miaka 30+ lkn hana mafanikio hata kiwanja lkn kazi huwa anapata na pesa yakutosha ila tatizo alilonalo ni anapenda sana starehe!
waswahili husema "ukubwa wa pua si wingi wa makamasi"
unaweza kuwa mkubwa kiumri lkn bado haujajitambua!.

kwanini niseme kujitambua ndio chanzo cha mafanikio..?
kwasababu..
ukijitambua utajua nini ufanye na kwanini na kivipi ili ufikie malengo yako ambapo ndio mafanikio yako.
ukijitambua utajitambua wewe ni nani na unatakiwa ufanye nini ili utimize malengo yako.. mbali na hapo mtu asiejitambua hajui afanye nini na kwanini.. hii ni sawasawa na bure! wengine husingizia kurogwa! huu ni upuuzi wakutupwa kama haujajitambua hautatambua mafanikio utayaona kwa wengine tu.

Bora tujibidiishe ktk kutoa elimu ya kujitambua hapa nafikiri watafunguliwa wengi.. mtu ana kitu lkn hajajitambua kama anakitu lzm atabaki kutokuwa na kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…