Kujenga Daraja la Busisi-Kigogo, Hospitali na Uwanja wa Ndege wa Chato ni Kuigawa Nchi, ni ubaguzi na ubinafsi wa Magufuli unaoendelzwa Rais Samia

saigilomagema

JF-Expert Member
Jun 5, 2015
4,522
7,030
Hii miradi iliyoigharimu na inayoendelea kugharimu Taifa letu ni miradi ambayo imeigawa hii nchi vipande, ni miradi ya kibaguzi, yenye ubinafsi wa hali juu.

Ni miradi ya matrilioni ya pesa za walipa kodi maskini wa nchi hii wanaoishi ndani ya nchi maskini ambayo ina mitandao ya barabara za vumbi bado.

Kiukweli tukiacha ubinafsi nchi yetu badi haijafikia uwezo wa kupitishia barabara juu ya bahari au ziwa kwa urefu wa mpaka kilomita 3 ma mita 200, huu ni ulimbukeni ni matumizi mabaya ya kodi ya wananchi maskini, ni ubinafsi wa kiongozi na vipaumbele vya hovyo kisa tu kiongozi ametokea upande huo wa nchi. Hii ni dhambi kubwa sana itakayoitafuna nchi vizazi na vizazi sijui nani wa kuja kutuponya.

Daraja la Kigogo-Busisi inaunganisha wilaya ya Misungwi na Sengerema zote ndani ya mkoa moja wa Mwanza na wala haina magari mengi mi nimepitia pale mara kadhaa.

Kuna vivuko viwili na vinatosha kabisa. Mwendazake alijenga hoja eti wamama wanajifungulia njiani, uwongo mtupu kukatiza pale haichukui zaidi ya dakika 15. Je hawa wanaopitia barabara zilizojaa mashimo na mawe siyo binadamu? siyo watanzania?

Mwezi wa 9 wakati natokea Loliondo kuelekea Arusha basi ilipasua matairi yote mawili ya nyuma ya upande moja kwa wakati moja tulitembeleana ringi kwa mita kadhaa basi lilikuwa na abiria zaidi ya 60 ilikuwa tuangamie pale kama siyo mkono wa mwenyenzi Mungu.

Magufuli aliwagawa watanzania wale wa upande aliotokea yeye daraja la juu wanaostahili maendeleo wa kanda zingine watwana tu hawawezi kuumia wabaki na tabu zao.

Nchi hii kwa sehemu kubwa barabara zake nyingi hazipitiki ni za vumbi. Mifano michache ni kama ifuatayo: Barabara kutokea Handeni-Kilindi(Tanga)-Kiteto(Manyara)-Kondoa na Kongwa(Dodoma) ni Vumbi. Barabara kutoka Arusha-Simaniro-Kiteto(Manyara) Vumbi. Barabara kutokea Ifakara-Mahenge-Malinyi(Morogoro)-Ludewa(Njombe) vumbi. Barabara kutoka Karatu(Arusha)-Mbulu-Haydom(Mbulu-Manyara)-Nduguti(Mkalama-Singida)-Ibaga-Sibiti(Singida)-Mwanhuzi(Meatu)-Maswa(Simiyu) vumbi. Barabara kutoka Karatu(Arusha)-Matala-Meatu-Bariadi(Simiyu) vumbi. Barabara kutoka Mto wa Mbu(Monduli-Arusha)-Loliondo-Mugumu(Serengeti-Mara) vumbi. Hizi ni baadhi ya barabara kubwa zinazounganisha wilaya kadhaa iliyoko katika mikoa tofauti kama ilivyooneshwa ktk brackets ambako kuna shughuli nyingi sana za kiuchumi na kuna wananchi wengi sana.

Mwananchi anayetokea maeneo haya akifika Dar es Salaam anakuta ma-flyovers, anakuta barabara zimepita juu ya bahari kama daraja la Tanzanite hawezi kuamini kama bado yuko ndani ya nchi ileile moia inayoitwa Tanzania.
Ndiyo maana Dar Es Salaam itaendelea kujaa raia kwani kijana ambaye hajaacha majukumu yoyote alikotokea hawezi kurudi atabakia Dar ushahidi ninao. Nani anataka shida?

Leo ndani ya nchi ile ile mtanzania anakuta barabara yenye urefu wa km 3 na mita 200 imepitia juu ya ziwa imejengwa kwa bilioni 700 baada ya kuondoa kodi, pamoja na kodi gharama inafikia kwenye trilion.

Huu kama siyo ubaguzi na kuigawa nchi ni nini? Samia Rais wetu wa sasa na Waziri mkuu wako tunajua kama siyo Magufuli msingekuwa hapo mlipo ila mnalipa fadhila za marehemu kwa gharama kubwa sana ya damu zetu watanzania.

Kila mara mko kanda ya ziwa hamieni kabisa huko kwanza rais umeshatuambia una ploti Chato kajenge uwe karibu na kaburi la Magufuli. Mbona hujawahi kutembelea kaburi la baba wa Taifa au kwasababu siye aliyekupa ulaji? Unaendeleza ubaguzi ule ule wa Magufuli.

Watu tunalaani kwa nguvu zote ubaguzi na alioupandikiza mwendazake we unaupalilia. Unatuangusha sana Rais wangu.

Wale wa povu karibuni, wa kutukana mpo huru kama anavyosemaga mwenda zake message sent and delivered. Mimi kwetu Tunduru kijiji cha Kazamoyo takribani kilomita 70 kutokea mjiji Tunduru unaweza kuanzia safari Tishari ya Kafu kupitia vijiji vya Azimio, Semeni, Mtina, Lukumbule na hatimaye kwetu Kazamoyo.

Barabara yetu in ya vumbi nauli sh. 7000 kutoka Tunduru lakini bado haifikii kwa umuhimu barabara tajwa hapo juu maana hizo zaunganisha mikoa.
 
EfKjCp3X0ActKyg.jpeg
 
Hii miradi iliyoigharimu na inayoendelea kugharimu Taifa letu ni miradi ambayo imeigawa hii nchi vipande, ni miradi ya kibaguzi, yenye ubinafsi wa hali juu...
Rais SSH lazima aimalize yote hata kama ilikosewa kwa vile tayari kuna uwekezaji Mkubwa sana wa fedha za umma.

Kama angeiacha siyo tu angekwamisha uchumi Bali angeonekana ana SABOTAGE miradi iliyoasisiwa na mtangulizi wake.

All in All Magufuli alikosea na kukurupuka kuanzisha miradi mikubwa bila FEASIBILITY STUDY na ndiyo maana AMEKUFA kabla HAJADIDIMIZA nchi kiuchumi na kuigawa KIITIKADI na KIKANDA na KIKABILA
 
Rais SSH lazima aimalize yote hata kama ilikosewa kwa vile tayari kuna uwekezaji Mkubwa sana wa fedha za umma.

Kama angeiacha siyo tu angekwamisha uchumi Bali angeonekana ana SABOTAGE miradi iliyoasisiwa na mtangulizi wake.

All in All Magufuli alikosea na kukurupuka kuanzisha miradi mikubwa bila FEASIBILITY STUDY na ndiyo maana AMEKUFA kabla HAJADIDIMIZA nchi kiuchumi na kuigawa KIITIKADI na KIKANDA na KIKABILA
Feasibility study ya nini tena mkuu. Sio kila jambo lifuate protocol sometimes unajiamulia tu
 
Wanataka kila kiwe dar tu hilo daraja litasaidia sana sana tu hakuna mambo ya kuvuka tena
Hiyo busisi nina wasiwasi hata kama ameshawahi kufika na mtu anaeona mwanza inapendelewa nashindwa kuelewa

Mwanza ni kubwa next to dar Ila miundombinu ya dar na mwanza unaweza kuifananisha. Barabara zenyewe tu mtihani na airport ambayo haiishi

Watu bhana 😡😡😡
 
Hiyo busisi nina wasiwasi hata kama ameshawahi kufika na mtu anaeona mwanza inapendelewa nashindwa kuelewa

Mwanza ni kubwa next to dar Ila miundombinu ya dar na mwanza unaweza kuifananisha. Barabara zenyewe tu mtihani na airport ambayo haiishi

Watu bhana 😡😡😡
Chuki ni saratani!
 
Back
Top Bottom