ingekuwa vyema sana kama utumishi ndio wangeendesha hilo zoezi la usaili.
acheni kulalamika ndugu ...kafanyeni usahili then mtajua......Dahhh,ww acha kk,yani hapo ni sheedah tupu,anyway watakaobahatika watoto wa masikini waende huenda Allah akaleta wepesi ktk hilo
Ninavyojua Hawa vijana walioitwa hawatakosa cha Kujitetea mfano Zile hesabu Ngumu Sana!
Mbona ni rahisi tu, kama wanapenda ni tatizo lao, sio lako..we fanya umeme wako na hiyo mechanical.Aisee hili imeshakua tatizo.. sijajua kwanini vijana wenzangu wanapenda sana kusoma masomo kama ya computer wakati unataka ajira? jamani bado kuna kozi kama Mechanical au Umeme bado watu ni wachache japo fursa siyo nyingi sana.
Sasa hiyo nyomi kwa waoga lazima warudi nyuma na matumaini inazidi kupungua; fani kama umeme unaweza kuasidiana na wenzako ukawa unapanda darini kufanya wiring
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA MCHUJO (APPTITUDE TEST) VITENDO (PRACTICAL) NA MAHOJIANO (ORAL INTERVIEW)
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), inatarajia kuendesha zoezi la Usaili wa Mchujo, Vitendo na Mahojiano kwa Waombaji Kazi waliotuma Maombi kufuatia Tangazo la Kazi la Tarehe 10 Machi, 2017 kwa ajili ya kujaza Nafasi Mbalimbali za Kazi.
Majina yako kwenye website ya TPA (ports.go.tz) au kwenye document hapo chini:
mmmh! sasa utapewa mtihani wa hesabu hata kama umeomba nafasi ambayo haihusiani na hesabu!!!!!!Ninavyojua Hawa vijana walioitwa hawatakosa cha Kujitetea mfano Zile hesabu Ngumu Sana!
wewe umejuaje??.. wakuu mbona kada zingine kama records assistant hazionekana .. naona wameita post za ict tu..? mwenye taarifa atujuze tafadhali..