Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,121
- 120,354
Wanabodi,
Declaration of Interest
Bandiko hili sio la kujidai na kuonyeshea Wasukuma ni matajiri sana, na tunapanda sana ndege, bali ingefanywa sensa ya ni kabila gani linaloongoza kwa kukwea pipa kwenye domestic routes na route ya Mwanza ndio cash 🐄 wa mashirika ya ATC, Fast Jet na Precision, bali Wasukuma tunakwea sana pipa sio kwa sababu ni matajiri sana, bali tunakwea sana pipa kwa sababu Kanda ya Ziwa ndio Kanda tajiri zaidi Tanzania, na Wasukuma ndilo kabila tajiri zaidi kwa utajiri wa roho, ndio ma spenders wakubwa, kulipia ndege kwenda kusalimia sio issue sana, japo tatizo letu ni ushamba tuu, ila ndio watu wa matumizi.
Kuna huu msemo, kizuri kula na mwenzio, ila huu sasa ni msemo wangu, "Yakikuta ya Kukuta" waonye na mwenzio ili yasiwakute kama yaliyokukuta wewe. Mimi mwenzenu leo yamenikuta ya kunikuta, hivyo hili ni bandiko la kuwaonya wengine wenye tabia kama zangu, kubadilika ili yasiwakute ya kuwakuta.
Ndege yetu ya Dreamliner ni kubwa na ndege nzuri, hivyo ulipopitishwa uamuzi wa kuinunua, tulisema mengi humu, Hakuna abiria wa kushindanisha kwa "afya" mashirika matatu ya ndege kwa safari za ndani - JamiiForums
Baada ya taarifa kama hizi kuwa dreamliner haitajaa, hivyo baada dreamliner kuwasili, sisi Wasukuma wa Mwanza, tuliojaaliwa kidogo, tulikuwa tunajidai sana na ndege hii, sometimes hata bila sababu yoyote ya msingi, tulikuwa Ijumaa tuu, ikitokea umepiga deal lako na uko fresh, unaamua kesho asubuhi nakwenda zangu Mwanza kusalimia, nitarudi jioni, na kutokana na kila siku kukuta Dreamliner haijai, sikuwa tena na haja ya kufanya booking yoyote, wewe ni kwenda tuu pale airport on time, unakata tiketi yako na kupanda ndege, kama tuu unapanda dala dala.
Ukijenga mazoea, yanageuka tabia, haya mazoea ya kutofanya booking mapema, na kujiendea tuu airport kujipandia Dreamliner kwa sababu kila ukipanda unakuta haijai full, ilikuja kuwa ndio tabia yangu, na kwababu mwanzo prices zilikuwa fixed, nikajenga tabia, ya ukitaka kusafiri na dreamliner, huna haja ya kufanya booking mapema, sasa leo kuneniponza na hapa nilipo, tayari nimeisha kwama jijini Mwanza!. Mazoea mabaya ya kutofanya booking mapema kumeniponza, nimekosa nafasi, ndege zote za Mwanza Dar, zimejaa full mpaka Jumanne!.
Nimekuja hapa Simiyu kwenye Maonyesho ya SIDO, maonyesha yanaisha leo saa 8:00 mchana, natakiwa kwenda Mwanza kupanda ndege kurudi Dar, kuwahi Maonyesho ya Viwanda Kibaha yanayoanza kesho. Sasa kama kawaida yangu, with Dreamliner isiyojaa in mind, nimepanga baada tuu ya kufungwa kwa maonyesho, naondoka kwa gari na kwenda Mwanza, straight airport kupanda Dreamliner, si najua huwa haijaagi!, sasa leo ni kama Mungu tuu, na hivi vibranketi vya Bariadi, vyepesi, unaweza kujifunika, na bado ukapigwa baridi, hivyo baridi ya asubuhi ikanikatisha usingizi wangu mapema, nikaamua kucheki stutus ya online bookings, nilichokikuta, sikuamini macho yangu kukuta ATC iko full!, sio leo tuu, iko full mpaka Jumanne!, Hii maana yake kazi ninamaliza leo, nitalazimika kukaa siku mbili mzima Mwanza, kisa kuitegemea Dreamliner kuwa huwa haijai, jameni leo mwenzenu, nitaumbuka!.
Tangu ujio wa Dreamliner, Fast Jet na Precision niliziona kama taka taka, sikuwahi tena hata kuziwazia, tena kuna kipindi nilishangilia kifo cha Fast Jet kwa kisingizio cha uzalendo wa ATC, ATC Sasa Yaanza Kuleta Heshima ya Nchi, Yapunguza Tanzania Kufanywa Shamba la Bibi, FastJet Yapumulia Mashine, Soon Itafungasha Virago!. - JamiiForums
Pia niliwahi kuizungumza hivi Precision Air Uchumi wa Magufuli: Precision Air Yapumulia Machine. Yapunguza Wafanyakazi 136! - JamiiForums
Hivyo baada ya kukwama kupata ATC, leo ndio nimeikumbuka Fast Jet, nayo imejaa mpaka Jumanne!. Nimeikumbuka hadi Precision ambayo niliidharau kuuita pangaboi, kuwa "nani apande pangabio mahali kwenye jet?", leo hata hilo pangaboi nalo nimeikuta limejaa mpaka Jumatano!. Nitafanyaje jameni, mwenzenu nimekwama!.
Kiukweli hapa nilipo, nimechanganyikiwa, kwa sababu, nina kazi muhimu kesho asubuhi kule Dar, kuchanganyikiwa huku kuninifanya hadi niwaze kuwafuata wale Wazee wa Gamboshi, kutumia ule usafiri wao, nasikia unakalishwa mahali, unaambiwa funga macho, dakika moja tuu ukifungua, unajikuta uko nyumbani kwako, chumbani kwako, tatizo la usafiri huu ni masharti yake, sharti lake kubwa ni kwanza lazima usafiri huku umevaa ile birthday suit yako, kisha unapakwa mafuta fulani, na hutakiwa kufungua macho mpaka ufike!. Hili la kuvalia birthday suit kwa umri huu lataka moyo!.
A Way Forward.
Kwa vile haya mambo ya kuambiwa ndege ni full haina nafasi, lakini nipoenda ofisi zao za Airport, nikapata nafasi na ndani bado kukawa na two more empty seats, supposedly, kulitokea no shows tatu kama ilivyonitokea hapa Ushauri wa Bure kwa ATC: Anzisheni frequently fliers na fanyeni over booking kwa waiting list. - JamiiForums
Kwa vile huwa kuna uwezekano wa kutokea no shows, na sisi binadamu tumejaaliwa uwezo wa kufanya lolote kupitia the power of mind, hivyo sasa leo sitasubiri tuu mpaka hiyo no show ijitokee tuu by chance, bali sasa, kutokana umuhimu wa kusafiri leo, leo nitalazimika kutumia will power, kulazimisha kutokee no show, ili niweze kusafiri.
Somo.
Tuache kuishi kwa mazoea, tujifunze ku plan ahead, tangu namaliza Nane Nane ya Simiyu ile mwezi wa 8, nilijua kuhusu maonyesho haya na tarehe kufungwa kwa maonyesho haya, sasa nini kilinifanya nisifanye booking mapema kisa kuibwetekea dream liner kwenda kupanda ndege kama kwenda kituo cha daladala.
Ila pamoja na yote haya, jee kweli hizi full flight ya ATC Jumapili na Jumatatu, at the same time Fast Jet nayo pia iko full, Precision nayo pia iko full, hii full ya ATC ni dreamliner kweli?, au walikuwa wanatuonjesha tuu dreamliner, sasa ndio imeanza safari za ki dreamliner za kiukweli ukweli, if not, dreamliner yetu iko wapi na inafanya nini?.
Niombeeni niweze kusafiri leo, nikifankiwa nitarejea kutoa mrejesho wa the will power, nikikwama pia nitasema, japo kulala Mwanza nako kuna raha zake haswa vile vibaridi baridi vya Ziwa Victoria vinafanya ujifunike blanketi ukijusha na sato wa Mwanza fresh from the lake... kazi inaweza kusubiri.
Nawatakia Jumapili Njema,
Msikose kuangalia kilele cha maonyesho ya Sido Simiyu ambayo yatatangazwa live na TBC kuanzia saa 5:00 Asubuhi hii.
Paskali
Update.
Jana nilifanikiwa kusafiri, kulitokea no show moja, nikapata nafasi japo pia mfuko ulitoboka vilivyo (half 6 figure),
Ndege ni dreamliner, na limejaa, Fast Jet, pia ilikuwepo na imejaa, Precision pia Ilijaa!.
Kwa hali, ilivyokuwa pale Mwanza Airport jana usiku, nikisema Wasukuma ndio wanaaongoza kupanda ndege nchini, nitakuwa nimedanganya?. Simaanishi abiria wote wanaopandia Mwanza ni Wasukuma, bali walio wengi ndio hao
Asanteni kwa maombi yenu.

Nina wasiwasi kama Dreamliner yetu itapata abiria wa kutosha safari za ndani na nje. Huu ni ushauri wangu kwa ATC. - JamiiForumsChangamoto kubwa itakayoikabili Aviation Industry hapa nchini kwa sasa ni uchache wa abiria utakaosababishwa na mambo kadhaa nitakayoyaanisha hapa chini kulingana na mtazamo wangu huku mashirika ya ndege yakiendelea kuongezeka kila kukicha.
Wakuu, ukweli ni kwamba tangu suala la kuagiza Dreamliner lilipotangazwa, niliingiwa na wasiwasi sana juu ya uwezo wa ndege hii kujaza abiria kwa safari za ndani na nje.
Wasiwasi wangu umezidi kuongezeka niliposikia kuwa hata baada ya matangazo mengi juu ya kuanza safari za ndani kwa ndege hii na nauli ya chee, imeshindwa kujaa kwa safari yake ya kwenda Mwanza na kurudi. Uwezo wa Dreamliner ni kubeba abiria 262. Hadi sasa safari ya Mwanza ya asubuhi ni abiria 244 na ya mchana abiria 158. Ikumbukwe kwamba mara nyingi safari ya kwanza huwa inakuwa na hamasa kubwa na abiria hupatikana kuzidi uwezo wa ndege.
Sasa je, hizi ni dalili kwamba huko mbele tunaweza kuwa na tatizo la kujaza ndege yetu kwa safari za ndani au nje? Uwezekano huo upo, na ATC wanapaswa kulikubali hilo. Je, tumenunua tembo mweupe?
Sidhani kama kuna lolote tunaweza kufanya kwa safari za ndani zadi ya kushusha bei hata zaidi kama "promotional fares". Ni afadhali ushushe nauli ili upate abiiria wengi katika kile wachumi wanaita "economies of scale".