Kwa mbali nakiona kiburi cha wanasiasa kutaka kutumia kete ya mradi huu kuzidi kujijenga kisiasa. Naamini wataalamu walishafanya tafiti zao na kutoa mapendekezo ya namna bora ya kuuendesha mradi huu hasa kwenye hatua ya mwisho kabisa ya "Mtumiaji" au "Mlaji".
mradi huu lengo lake ni kupunguza adha ya foleni iliyokithiri kwa muda mrefu jijini Daresalaam ambayo kimsingi inasababishwa na ongezeko kubwa la magari na idadi ya watu ambao kila siku, saa, dakika na sekunde wanahitaji huduma ya usafiri kutoka eneo moja kwenda jingine kwa ajili ya kujitafutia kipato.
naomba nijadili haya mambo makuu mawili;
Ongezeko kubwa la magari: hapa ni dhahiri kwamba mradi huu utawavutia wafanyakazi wanaotumia magari yao kwenda kazini na kurudi kwa mantiki ya kukwepa adha ya kubanana kwenye daladala, kuchafuka, hewa mbaya, kuibiwa, kusimama na kadhalika. uzoefu unaonyesha kwamba wafanyakazi hawa matumizi yao makubwa ya gari zao ni kwenda na kurudi kazini na mara chache hutumia kwenye mambo mengine mara baada ya kazi ikiwa ni pamoja na kwenda sokoni, kupitia kwa marafiki na mengine mengi. Kwa mantuki hiyo ni wazi kwamba mradi huu utawafanya wafanyakazi kutoona ulazima wa wao kutumia usafiri wao na kuamua kutumia huduma ya usafiri ya mradi huu huku kukiwa hakuna adha zozote ambazo zitawafanya wao kujutia kutumia usafiri huo. Hii ni endapo tu mradi utetekelezwa kadiri wataalamu walivyoshauri na wanavyoendelea kushauri.
Idadi ya watu: hii imepelekea kupanuka kwa makazi na iuhitaji wa huduma za kijamii ikiwa ni pamoja na usafiri. Naamini watu wengi wanashauku ya kuanza kutumia usafiri huu wa mradi wa mabasi yaendayo kasi lakini suala la usafi, mizigo, mifugo na mengine mengi vinatakiwa kuangaliwa kwa jicho la pekee na hapa ni utashi tu wa kisiasa unatakiwa kuonekana vinginevyo ni kuua mradi.
tunajua serikali inawajali wananchi wake na inawathamini sana lakini kwa hili ni vizuri serikali itamke tene pasipo kumung'unya maneno kwamba hataruhusiwa mtu kupanda na mizigo kama samaki, magunia ya mboga, nyanya, mbuzi, kuku, na mizigo mingine kama ambavyo tumezoea kuona kwenye daladala.
chonde chonde nashauri na tena naonya kuingiza siasa kwenye mradi huu ni kuua lengo kuu la mradi.