Kuikumbatia UCHINA ni janga la Taifa

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,745
fikiria wachina waliofika kuuza mahindi ya kuchoma ndani ya jiji hata kufikia kuuza mafenesi pale mjini Muheza ,wachilia mbali kuingia katika biashara za vipusa ,but they dont care about us ,hilo mlijue.

Wachina wauza karanga na kwa jinsi tunavyowaonyesha paja ndivyo watakavyotaka tunyanyue nguo kamili ,kwa maana hiyo WaTanzania mjue biashara zenu zote watazikamata wao na hatutoweza kushindana kibei ,watauza bei poa kiasi ya wewe kula hasara na kuamua kumwaga manyanga ,leo hii wanajaliza biashara zao feki na huwapa wamachinga kuuza,hapa wanapima upepo tu ,muda si mrefu watauza wenyewe na hao wamachinga watabakia kufuta mavumbi bidhaa kwenye maduka ya wachina.

China ni Taifa lenye watu wengi na kwao hawana la kufanya siasa wanazotumia ni kuwasambaza wengine katika nchi za nje na huwapa kila msaada na kuwalinda kimaslahi ,tunapoanza kuitegemea China kimisaada basi mjue watatoa misaada kila rangi na kutudumaza akili kiasi ya kutufikisha kwenye point ambayo tutakuwa hatuwezi hata kuchamba bila ya kupata msaada wa kichina kwa msemo mwengine itakuwa tumeshanasa na tunakokotwa kama mbuzi anaegoma kuvutwa kamba.

Serikali inaona imepata kuwa ina/itapokea misaada kutoka china kumbe bila ya kuona mbali itakuwa imepatikana.
 
China ni taifa janja sana. Tena tukizubaa watakuja mpaka kuanzisha chama cha siasa, na kusimamisha wagombea kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge na uraisi. Sasa wameanza na kampuni za ulinzi, kuuza karanga n.k
 
China ni taifa janja sana. Tena tukizubaa watakuja mpaka kuanzisha chama cha siasa, na kusimamisha wagombea kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge na uraisi. Sasa wameanza na kampuni za ulinzi, kuuza karanga n.k
Kuweni na shukrani basi kila kitu ni kukosoa tu, ingekuwa USA bado mngesema. Fanya kazi kijana acha kutegemea miujiza tafuta fursa ilipo.
 
Tatizo ulisoma ukitegemea kazi serikalini ila ukasahau ata kujiajiri ni kazi. Wachina ata kama mtu ana degree haoni aibu kufungua kibanda cha chips kama ameona kunafaida. Acha kulalamika fanya kazi.
 
Kuweni na shukrani basi kila kitu ni kukosoa tu, ingekuwa USA bado mngesema. Fanya kazi kijana acha kutegemea miujiza tafuta fursa ilipo.
Shukurani kwa lipi ? umegusa kitu FURSA sasa hizo ndio zinazokamatwa na waChaina ,unapokwenda unawakuta ,embu angalia wapo Muheza wanauza mafenesi ,inaonyesha huishi Tz kwa miaka mingi ,sivyo ulivyoiacha ,hebu rudi kwenu bodaboda dereva ni mchina na wanasema ni more safe.
 
Tatizo ulisoma ukitegemea kazi serikalini ila ukasahau ata kujiajiri ni kazi. Wachina ata kama mtu ana degree haoni aibu kufungua kibanda cha chips kama ameona kunafaida. Acha kulalamika fanya kazi.
Sasa wakafungue huko kwao kwanini waingie ndani ya nchi na kufanya biashara sa kuuza miogo ya kuchoma na kukaanga na zaidi wanauza rahisi kupindukia huwezi kushindana nao ,hasara wanalipwa na serikali yao je Mtz ataweza kulipwa na serikali ?
 
Haya Mkuu nimekuelewa ila inatupasa kushindana na hizo changamoto badala ya kulalamika .wao wamekuja kutafuta fursa kwetu kwa sbb wameziona kwann sisi hatukuziona before. Muheza hakuna vijana wa kuuza hayo mananasi?, tatizo tunaweka aibu mbele ktk kazi na kuwaza Maisha mazuri bila kazi, hakuna miujiza zaidi ya ubunifu na kuacha fikra tegemezi.
 
China ni taifa janja sana. Tena tukizubaa watakuja mpaka kuanzisha chama cha siasa, na kusimamisha wagombea kuanzia udiwani, uwakilishi, ubunge na uraisi. Sasa wameanza na kampuni za ulinzi, kuuza karanga n.k
Nimecheka kweli yaani hadi ulinzi china, midori, china njiti za meno china, piki piki ajira ya Makonda china, Nywele feki bandia china, mkorogo china , makalio makubwa china (wakati wenyewe ni pasi) china jamani hata mayai feki, china.
 
Uku kariakoo ndo wamejazana kibao wanauza bidhaa bei rahisi kweli alafu wazawa tunaumia
 
Hamna MAGU awezi kuwakumbatia wachina uwoni miradi yote mikubwa miwili ambayo naifahaumu hiko hapa dar es salaam tumewapa wajapani
 
Acha uoga wewe, hizo ni cost ndogo za urafiki wa kweli kama vile wanavotusomeshea watu 150kila mwaka,

Wao wanashida zao na sie tuna shida zetu its win-win situation and not win-lose situation kama kwa wazungu!
Wazungu wanatuona ss waafrika mabogasi kbs, wachukue malighafi zetu wakazifanyia kazi Asia, Asia wakauze bidhaa Ulaya/USA na Afrika ila faida kubwa wapate wao kwa sbb wamewapa teknolojia, waAsia wapate kidogo ss tupate negative

Bora mchina, Ambaye yeye ss anataka kuwekeza kwenye teknolojia zaidi, so anatafuta masoko ya Viwanda vyake sio masoko ya bidhaa alizozalisha! ss akiangalia waAsia wenzake hawamkubali kiviile kwa sbb washashikwa na mmarekani, so akiweka viwanda vyake Afrika itakuwa faida kwake na kwetu pia!

The only way, kwa Afrika kuenda mbele ni kuwa na viwanda vya kujitosheleza, na mzungu hawez kujenga viwanda Afrika hata kwa dawa

Tumkubali tu Mchina, tutagain zaidi kuliko USA/Europe
 
dist111 ,upo mbali sana kuielewa siasa ya china ,yeye haoni tabu kuisomesha tz nzima ,ila uelewe hata akikosemesha hutoweza kushindana nae,labda muje kuwafukuza hapo baadae ,unasoma kwa kutegemea fursa ,fursa ambayo wewe ukimaliza kusoma na kurudi unawakuta wachina wamechooka wapo kila pembe wanaifanya ile kazi uliyoenda kusomea ,hawa wachina ni watu hatari sana ,hivi unawajua viwavi jeshi au wale ndege waitwao kweleakwelea ,ndo walivyo wachina wanajaa mpaka inakuwa uchafu na sehemu zote za biashara wanazikaa wao ndio kama wanazihozi wao kuanzia kuuza mafenesi hadi kutembeza maji ,shee mchina anatembeza maji mzegamzega ndani ya jiji la dar kama haitoshi kama una hela unamlipa kama huna anakwambia kesho tutalipa ndio utamlipa.
 

Mkuu, kuna mambo ya ajabu sana yanaendelea. Kuna zile receiver za zamani kabla ya hizi za kulipia zilikuwa zinaandikwa made in China. Ila ukiscratch hayo maandishi unakuta ni kikaratasi tu ndani kuna made in Korea. Niliuliza nikaambiwa bidhaa za China zinalipishwa kodi ndogo na hazicheleweshwi bandarini. Sasa unafiikiri unaweza ukashindana na watu kama hawa?
 
Nina wasiwasi na hii kamatakamata ya machngu doa na makahaba ,si ajabu wanataka kupewa nafasi wachina na wapo na zipo nchi wamejaa makahaba wa kichina sasa kulivaa soko la Tz lazima wazalendo wavunjwe kasi tusubiri tuone na nasikia zipo sehemu dar wapo wachina,
 

Wao sio wamekua kutafuta huko kwao wamejaa kuliko madai na hawana la kufanya ,sasa wanapokuja hapa husemi kama wameziona kuna fursa bali wanakuja kuwaharibia soko wazalendo ,kama unauza hindi la kuchoma mia tatu ,mia tano yeye atauza hamsini ,mia na atakuongezza jingine na limau na ndimu free ,hawa jamaa ni hatari unaweza kuwaita wachafuzi.
 
Walipomaliza kujenga reli ya TARAZA tuliwasifu kweli kuwa ni wenzetu. Walipotujengea uwanja wa mpira wa taifa tuliwapa sifa kemkem tukitaka na mikoa mingine vijengwe viwanja kama hicho. Sasa baada ya sifa hizo zote ghafla bin vuu tumeanza kuwageuka tena!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…