kuifanya ndoa yako kuwa bora zaidi na imara hebu zingatia haya machache

Genius Man

JF-Expert Member
Apr 7, 2024
806
2,049
uzi huu nikwaajili ya watu wote yani wale waliopo kwenye ndoa na hata wale ambao bado hawajaingia kwenye ndoa hebu zingatieni vitu hivi ili kuifanya ndoa yako kuwa bora na yenye furaha zaidi, ndoa yenye amani, upendo, uvumilivu, kujali, kusaidiana, kusikilizana, kuelewana n.k

kulingana na kuongezeka kwa migogoro kwenye ndoa tunajifunza nini sisi kama wanaume au wanawake ni vitu gani ambavyo tunapaswa kuvizingatia ili kushinda migogoro ya namna yoyote kwenye ndoa zetu hivi leo, sasa hapa kuna vitu baadhi vya kuzingatia ambavyo naamini kwa namna moja au nyingine vitaenda kukusaidia kuepukana na migogoro hii ya ndoa kwa wale mliopo na ambao mnajiandaa kuingia kwenye ndoa.


MWANAUME
Kwa wanaume wote wanao jiandaa kuingia kwenye ndoa au ambao wapo kwenye ndoa zingatieni vitu hivi ili kutatua migogoro yoyote itakayo tokea kwenye ndoa yako.

  • Kuwa mtu mkweli kwenye ndoa, mwanaume unapaswa kuwa mkweli kwenye ndoa yako hii itachochea upendo zaidi na kupunguza uwezekano wa migogoro kwenye ndoa yako.
  • Mpendelee zaidi mkeo, kwa wale wanaume mnao jiandaa kuingia kwenye ndoa na wale mliopo kwenye ndoa mnatakiwa kuwapendelea zaidi wake zenu kwenye vitu mbalimbali kwenye ndoa yenu hii itasaidia kuondoa migogoro kwenye ndoa hali itakayopelekea kuchochea upendo na uimara wa ndoa yako.
  • Kuwa mtu wa kumsikiliza, kumjali na kumuelewa mkeo, Mwanaume unapaswa kuwa mtu wa kumsikiliza na kumuelewa mkeo hii ni muhimu sana kwenye kuepukana na migogoro kwenye ndoa hali itakayo pelekea kuchochea upendo kwenu.
  • kuwa mtu wa kumsaidia angalau vikazi mkeo, mwanaume unapaswa kuwa mtu wa kumsaidia baadhi ya kazi mkeo muwapo nyumbani hii ni mbinu muhimu ya kuepukana na migogoro ya aina yoyote unapaswa kutenga kamda kidogo kumsaidia mkeo hii itachochea upendo zaidi kwenye ndoa yako.
  • Kuwa mtu mwenye sauti ya mwisho kwenye ndoa, Mwanaume unapaswa kuvaa uongozi kuwa kichwa cha familia na uwe na sauti ya mwisho kwenye kufanya maamuzi yote kwenye ndoa yako mwenyewe hii itasiadia kupunguza migogoro ya kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mwenye misimamo, mwanaume unapaswa kuwa na misimamo kwenye masuala mbalimbali ndani ya ndoa yako hii itasaidia kwa namna moja ua nyingine kuepukana na migogoro kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mwenye mahaba, mwanaume unapaswa kuwa mwenye mahaba hii itachochea upendo zaidi kwenye ndoa yako na kuepukana na uwezekano wa migogoro ya kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mwenye kufanya mazoezi na kula vizuri, mwanaume ili uwe na afya njema unapaswa uwe unafanya mazoezi na kula vizuri hii itaboresha viungo vyako nakuwa mtu mwenye uwezo mzuri hata wa kumridhisha mkeo hii itapunguza uwezeka o wa uwepo wa migogoro kwenye ndoa yako.
  • Kuwa mtu mpole na rafiki mzuri wa mkeo, mwanaume unapaswa kuwa mpole na rafiki wa mkeo hii itachochea upendo na kupunguza uwezekano wa migogoro yoyote kwenye ndoa.
  • kuwa mtu wa kumtunza mkeo, mwanaume unapaswa kijitahidi angalau kumtunza mkeo kwa kumtimizia mahitaji yake hii itachochea upendo na kupunguza uwezekano wa migogoro kwenye ndoa.
  • kuwa mtu wa kufanya kazi kwa bidii kufikia mafanikio, mwanaume unapaswa usiwe mvivu unapaswa kufanya kazi kwa bidii ili kupiga hatua kimaisha kufikia mafanikio hii inaweza kusaidia kwa namna moja au nyingine kupunguza migogoro ndani ya ndoa.
  • Kuwa mtu ambaye asiye mlevi kupindukia, mwanaume unapokuwa kwenye ndoa unapaswa usiwe mlevi kupindukia hii itasaidia kuepukana na migogoro kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mwaminifu, mwanaume unapaswa kuwa mwaminifu kwenye ndoa yako kwamba unahakikisha hauchepuki na unarudi nyumbani kwa wakati hii itasaidia kuboresha ndoa yako na kupunguza migogoro.
  • Kuwa mtu wa kufanya ibada, mwanaume unapaswa kuwa mtu wa kufanya ibada kuimbea ndoa yako angalau mara kadhaa ili kupata mibaraka kwenye ndoa yako hii itasaidia kwa namna moja au nyingine kudumisha ndoa yako na kuepukana na migogoro.

MWANAMKE
Kwa wanawake wote mnao jiandaa kuingia kwenye ndoa au mliopo kwenye ndoa hebu zingatieni vitu hivi ili kuepukana na migogoro yoyote inayoweza kuzuka kwenye ndoa yako.

  • kuwa mtu mpole, mwanamke unapaswa kuwa mpole kwenye ndoa yako hii itasaidia kuepukana na migogoro kwenye ndoa.
  • kuwa mtu asiye na tamaa ya aina yoyote, mwanamke unapaswa usiwe na tamaa ya aina yoyote hii itachochea upendo zaidi kwenye ndoa yako na kuepukana na migogoro kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mwaminifu, mwanamke unapaswa kuwa mwaminifu kwenye ndoanyako hii itachochea upendo kwenye ndoa yako na kuepukana na migogoro ya kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu asiye mlevi kupindukia,mwanamke unapaswa kuwa mtu asiye mlevi kupindukia hii itasiadia kupunguza uwezekano wa migogoro kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu wa kujali na kumsikiliza na kumuelewa mmeo, Mwanamke unapaswa kumjali, kumsikiliza mmeo hii itasaidia kwenye kuepukana na migogoro ya kwenye ndoa.
  • Timiza majukumu yako kwenye ndoa, mwanamke unapaswa kutimiza majukumu yako yote kwenye ndoa ikiwemo kufanya kazi za nyumbani, kupika, usafi, unyumba n.k hii itachochea upendo zaidi kutoka kwa mmeo na kupunguza migogoro yoyote inayoweza kutokea kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu mkweli, mwanamke unapaswa kuwa mkweli kwenye ndoa hii itasiadia pia kwenye kupunguza migogoro yoyote kwenye ndoa yako.
  • Kuwa mtu wa kujitolea. Mwanamke unapaswa kuwa mtu wa kujiotelea kwenye ndoa yako siku mmeo akikosa hela unaweza kujitolea kutimiza mahitaji ya nyumba sio kila kitu unamuachia mmeo hii itachochea upendo baina yenu na kupunguza uwezekano wa migogoro kwenye ndoa.
  • kuwa mtu mwenye heshima kwa mumeo, mwanamke unapaswa kumuheshimu mmeo hii itachochea upendo zaidi kwako na kuepukana na migogoro ya kwenye ndoa.
  • Kuwa mtu wa ibada, mwanamke unapaswa kuwa mtu wa kufanya ibada kuiombea ndoa yako hii itasaidia kwa namna moja au nyingine kuifanya ndoa yako kuwa imara zaidi na kuepukana na migogoro kwenye ndoa.
  • kuwa mtu wa kujituma na mchapakazi, mwanamke unapaswa kujituma na kuwa mchapakazi hii itasaidj kuepukana na migogoro ya kwenye ndoa.
 
tuseme mara ngapi kuwa hakuna kuoa!, kusikia kwa kenge mpk atoke damu puani
 
Ishi na mwanamke kwa akili.
 
Mwanaume
👉Ampende mkewe
Mwanamke
👉Amtii mumewe na kuwa mnyenyekevu.

Ni hayo tu, mengine uliyoyaandika
ni sarakasi tu.
Bila hayo mawili, hakuna ndoa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…