Kuibuka kwa wimbi la wajiitao mapunter twitter.

Vhagar

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
20,455
39,731
Kuwako kwa wimbi kubwa na la ghafla mtandao wa X (twitter) kwa wanaojiita mapunter.

Uchunguzi wangu...


Wanatabia kama za watu wa forex now kuonyesha wana maisha mazuri sana na wanapiga hela kwenye betting.

Mbili, code wanazotoa ni za kweli, bt kama ilivyo kwa wote mwisho wa siku huchezi ww uwanjani itategemeana na upepo mnaweza kuliwa wote.

Tatu, kutokana na ni kweli wote mnaliwa au kula ila wao hawategemei mikeka 100% ndio maana wanapush sana promo code na grp za kulipia.
Unajua inakuwaje? Hizi referral code ni kuwa wanapata commission kila mtu anapodeposite hela. Wanapata kati ya 2 - 5% ya kiasi ambacho mtu huwa anadeposite.

Usidanganyike na stake kubwa mkeka ni kweli umetoa ila sio kwamba kaweka kweli stake kubwa hivyo.
Anaweza kuweka buku odd 5 mkeka kweli utawin shilingi 5000.

Anachofanya anaedit anaonyesha aliweka mil 1. Na itaonyesha kawin mil 5.

kuwa makini bet kiasi unachomudu kukipoteza. Kamari si ajira.
Mbaya zaidi mtu asiye na kazi inamuondolea mpaka juhudi kutafuta ajira akiamini atatoboa kupitia betting.... Acha mara moja usidanganyike usikubali kuwa nyumbu.

Imeandikwa na mimi mwenyewe TROUBLEMAKER
1000083348.jpg
 
Back
Top Bottom