Kuhusu Zanzibar Mpendwa Rais Amekosea

Rulleger

Member
Aug 29, 2015
84
60
Jana katika Hotuba yake kwa wazee wa Dar Rais magufuli alitusisimua wengi (kama kawaida yake) kwa jinsi alivyodhamiria yeye na serikali yake kuondoa ufisadpi na kuleta maendeleo kwa watanzania wanyonge. Hata hivyo kuhusu Zanzibar amekosea. Amesema hataingilia. Anakosea kwa sababu nne:
1. Si kila mzozo, na hasa zaidi mizozo ya kisia inasuluhishwa kwa sheria. Pale sheria inaposhindwa kuleta haki au kuwafanya watu wajisikie wanatendewa haki basi mazungumzo hufanyika ili pande zote zilidhike kwa ajili ya usitawi wa nchi na amani. Binafsi naunga mkono sana kurudiwa kwa uchaguzi. Sioni njia nyingine practical ya kumaliza mzozo huu. Hata hivyo CUF wanapaswa waridhie. Uchaguzi hauwezi kuwa wa chama kimoja.
2. Sheria zinawekwa na watu na zinabadilishwa mara kwa mara. Tuna tatizo la katiba na baadhi ya sheria zetu. Kwa sababu hiyo (inawezekana) watu hawajaenda mahakamani kwa vile wanajua uamzi wa mahakama hautatoa suluhisho sahihi.
3. Tume ya Uchaguzi iko huru na haipaswi kuingiliwa - huo ni mtazamo chanya sana na wakupongezwa. Lakini kwa upande mwingine tume inaongozwa na watu na sio malaika. Kwa mfano kama Salum Jecha alifuta matokeo kwa shinikizo au mapenzi yake kwa CCM, je hapo heshima ya uhuru wa tume itasaidia?
4. Kuna hatari (Rais asipoingilia kwa ushawishi) CUF wakasusia uchaguzi. Naiita hatari kwa vile yalitokea siku za nyuma tunayajua. Kuweka majeshi aisaidii sana. Amani ya kweli hailetwi na majeshi. Watu watakaa kimya kwa woga lakini hawatapendana, hawatashirikiana, hawatashiriki kutekeleza mipango ya maendeleo. Siku wakikosa uvumilivu damu inaweza kumwagwa na majeshi yaliyowazunguka!!! Mungu apishe mbali lakini jambo hili limetokea wakati wa Rais Mkapa. Sio hypothesis.
Utafiti wa Citizen (Magufuli impresses many after 100 days ) umeonyesha karibu 50% ya watanzania hawaungi mkono rais anavyoshughulikia suala la Zanzibar. Bado ana muda. Anaweza kufanya kitu.
 
kwani zanzibar ni cuf na ccm tu ndo vyama? Si kuna wale walikuw wanagombea tonge wakina hamad rashid ila cuf tumesema no fanyeni uchaguz na vyama vingine
 
Tatizo lililopo upinzani mnataka atoe tamko msikie mtazamo wake, HATOFANYA HIVYO. Behind the scene, sio kwamba amekaa tu, anashughulikia hilo suala, Mama Samia yuko bize na hiyo issue, kama mnataka rais aite waandishi alafu aseme, hiyo haitatokea kamwe. Atakaa kimya!
 
Magufuli amekua vuvuzela kwenye sakata la zanzibar.
Akae kimya kama alivyosema ila ajue mawe yatapiga mayowe.
 
Magufuli hana uwezo wa kushughulikia hilo la Zanzibar, maana halihitaji kukurupuka na yy ni champion mkurupukaji
 
Kama sisi tunavyojitolea kuwasuluhisha wengine e.g. S Sudan, Burundi, Kenya, DRC , Cote de Voire etc. INATAKIWA NA SISI TUSULUHISHWE TUSIONE AIBU. Wenzetu huko walipopata shida viongozi wetu walikwenda mbio kuomba kuwasuluhisha, lakini hapa nyumbani hao hao hawataki suluhu AJABU

Watawala wameshasema hawataki kutawaliwa na vyama vya hovyo hovyo unategemea Magufuli aseme nini zaidi.
 
Cuf tupo imara kabisa na hatuyumbishwi umoja wetu ndio silaha yetu nia yetu ni moja tu kumuondowa mkoloni mweusi
 
Kwa suala la Zanzibar JPM amebugi
Magufuli yupo sahihi kwa sababu hizi

1. Katiba ya Zanzibar haimpi uhuru na nguvu ya kuingilia mambo ya ndani. Maalim Seif na timu yake ndio waliopeleka pendekezo hilo ili kuikomoa Bara.

2. Tume ya uchaguzi imepewa uwezo wa kutohojiwa hata na Rais katika maamuzi yake. Hili ni pendekezo la Jussa ili kuidhibiti Bara isitie mkono.

3. Katiba ya Muungano inampa Rais mamlaka ya kuangalia usalama wa Jamhuri ya Muungano, kwa kutumia eneo hilo, Rais anaweza kuingia Zanzibar na kuhakikisha hakuna amani inayovunjwa.

Mlitaka Rais aseme nitashughulikia mambo ya ndani ya Zanzibar yanayohusu uchaguzi ndani ya tume wakati hana huo uwezo? Rais yupo straight ndo maana wanaopenda kusikia kauli za kupambwa hawazipendi.

Mwacheni Rais afanye yale ambayo yako ndani ya mamlaka yake. Vile vile tujifunze kusikia na kuyachambua yale anayesema hata kama hamyapendi.
 
Wewe unataka afanye nini?

Angesema serikali za JMT na SMZ zinaendelea kulitafutia ufumbuzi, nadhani inge sound better zaidi kuliko ya "nitaendelea kukaa kimya"....

Kwa sbb akikaa kimya mwisho wa siku ili iweje na unaona kabisa hilo ni tatizo?

Au angesema kwa haerufi kubwa tu kuwa, suluhisho la huko ni hilo la Uchaguzi wa
marudio, CUF shirikini au bakini na msimamo wenu wa kususia!!

Au angesema, nawashauri wanaona mambo huko Zanzibar hayaendi sawa sawa, basi tunazo mahakama zetu, waende huko ili wakapate tafsiri ya kisheria na kikatiba ya kinachoendelea na kufanyika huko. Hapa angekuwa ameitendea vyema busara yake!!

Pia, naomba ieleweke vyema hapa, kuwa, ufumbuzi ni pamoja na kuwashawishi CUF wakubali kushiriki uchaguzi.
 
"Ujinga ni kuendelea kurudia na Uchaguzi kwa Tume ileile na namna ileile huku ukitegemea matokeo tofauti"
- Albeit Einstein
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…