Ndg wanaJF,
Tumekuwa kwenye kipindi ambacho vyama vingi vya siasa hasa vile vya upinzani vikihubiri mabadiliko wakimaanisha kuleta mambo tofauti katika serikali yao ambayo chama tawala kimeshindwa kuyafanya kwa wananchi.
Lakini kinachonishangaza ni pale vyama hivyo vinapokosa kuleta mabadiliko ndani ya vyama vyao katika nyanja mbalimbali kama vile nafasi za uongozi, sera, dira, mfumo wa uendeshaji wa siasa za vyama pamoja na kutoa fursa kwa watu wengine ndani ya chama.
Je hatuoni kama kutuhubiria kutuletea mabadiliko kwa wananchi pindi mtakapopewa ridhaa ya kuongoza nchi ni UONGO mkubwa usiopaswa kuhubiriwa huku mkishindwa kufanya mabadiliko hayo hata ndani ya vyama vyenu?
MAWAZO HURU!