Kuhifadhi sumu ndani ni hatari sana

Kaunara

JF-Expert Member
Feb 4, 2013
237
421
Habari wadau!

Naandika habari hii kwa kuona kwamba kuna Sumu hatari sana kwenye maisha au jamii ya sasa zikiuzwa peupe bila mkono wa serikali kuingilia kati.

Watu wengi wamekuwa wakijtoa uhai kwa sumu mbalimbali mitaani kwetu na wengine wamekuwa wakinunua hizi sumu na kuweka ndani kwa kujua au kutokujua kwamba ni hatari.

Ushauri wangu usihifadhi sumu ndani ukishamaliza kutumia kwan ni hatari sana kwako na familia yako.

Mfano wa sumu. Dawa ya kukausha nyasi shambani, ni hatari sana kuhifadhi ndani hasa nyumba zenye watoto.

Sumu ya panya sio ya kuweka ndani kabisa. Hakikisha ukimaliza kutumia dawa yako ni bora hata kopo ukalitupa shimo la choo.

Naandika ujumbe huu baada ya mtoto wa familia moja kunywa sumu ya shambani na kufa Mbeya vijijini.

Nimeandika baadhi ya sumu ila kuna sumu haina nyingi sana mengine ni maua tunayopanda ndani ya nyumba niliona mama mmoja alichomwa na mwiba wa ua aliteseka sana mguu ulivimba sana.

Kama unajua baadhi ya sumu ambazo zijataja na hatari zipo mtaani embu elimisha jamii iwe makini. Kwa pamoja tuelimishe jamii.
 
Mwaka huu mpaka mwezi huu kabla ya mwaka kuisha nimepata kesi tisa za watu waliokunywa sumu za wadudu hivyo nawiwa kuunga mkono hoja yako .

Katika hao tisa ni wawili nilioweza kuwanusuru ila Saba walitangulia kutuwekea makao
 
Kweli kabisa
Baba aligoma kunipa sumu fulani, nilipokuja kuhoji akanipa semina hii hii
 
Mwaka huu mpaka mwezi huu kabla ya mwaka kuisha nimepata kesi tisa za watu waliokunywa sumu za wadudu hivyo nawiwa kuunga mkono hoja yako .

Katika hao tisa ni wawili nilioweza kuwanusuru ila Saba walitangulia kutuwekea makao
Hatari sana aisee inatisha. Wengine wanatupa makopo ya sumu kwenye vyanzl vya maji hawa hasa sumu za mashambani. Elimu kubwa inahitajika juu ya hili.
 
mengine ni maua tunayopanda ndani ya nyumba niliona mama mmoja alichomwa na mwiba wa ua aliteseka sana mguu ulivimba sana.
Sio maua tu kuna michongoma miiba yake ina sumu kali sana kuna miti fulani ipo porini watu wanaokaa shamba wanaijua ikikuchoma huponi sumu yake ni kali sana, kuna vile vimiba fulani vya baharini ukivikanyaga vina sumu kali sana lazima uvimbe mguu, nimetaja baadhi bila kusahau indosin sumu ya panya kiboko weka mbali na watoto
 
Simu Ni hiyo umefunga nayo ndoa.
Kweli kabisa, vijana watafute watoto tu mambo ya kufa na kuzikana hakuna, Ndoa zimekuwa za kuviziana mwanamke akishapata WATOTO ndani ya Ndoa na Ana kazi anahitaji Uhuru ukishindwa kumpa, Visa juu ya visa
 
Kutokana na ongezeko la changamoto ya afya ya akili, andiko hili ni la muhimu sana kuzingatiwa.
 
Back
Top Bottom