Tetesi: Kuhakiki TIN Mamlaka ya Mapato Tanzania ni shilingi 150,000

sabrynasri

Member
Jul 19, 2015
5
0
Habari wanajamii, leo alienda mtu nilimuagiza akakamilishe usajili niweze kupata leseni ya biashara niweze kuanza kazi kwani nimeshakodi fremu.

Nimepeleka picha ,mkataba wa pango, fomu niliojaza na vingine walivyohitaji, alipofika pale akahojiwa ili alipe kwanza kodi kabla ya kuanza biashara(nikaona huu wendawazimu inawekanaje sijaanza kazi uniulize nategemea kupata bei gani na nianze kwa kulipa kodi kwanza.

Jamaa akaona isiwe shida akakubali na wakakubaliana alipe sasa cha ajabu ni kuwa walimuuliza umehakiki TIN, akajibu hapana.

Nilikuwa nje ya nchi nimeingia wiki iliyopita basi wakamjibu anatakiwa alipie laki na nusu kuweza kuhakiki tin.

Sijui wenzangu mnalionaje hili suala? In short nimekataa kulipa hiyo hela na nimeshindwa kufungua biashara.
 

Uwe unafuata maelekezo na shurutis . Pengine timu walioajiriwa kuhakiki walisha ondoka nani alipie gharama za sasa?
 
Unamwamini uliyemtuma? Naomba tujue ofisi za TRA za wapi?
 
TIN hutolewa bure kwa mujibu was TRA kwa asiye kuwa nayo na hata zoezi la uhakiki halikuwa na malipo.

Sijui sasa kwa yule aliyetakiwa kuhakiki na hakufanya hivyo kwa muda ule ambao TRA ilitoa la uhakiki kupita kama anapigwa faini ama la.

Nadhani TRA wanaweza kuwa na majibu sahihi kama kuna faini au hapana
 
Mkuu mi waliniandikia tin no then wakapiga 2/cent ya mkataba na wakanikadiria kodi usilogwe ukasema biashara kubwa imekula kwako watakupa kodi kubwa
 
Dah hii hatari..sasa fedha zinakusanywa kwa style ile ya mkoloni wa kijerumani
 
Nchi ya viwanda hii duniani, kila kitu kiviwanda viwanda.
 
We fungua biashara wakikukamata utamalizana nao.
 
sasa kama kuna faini itakuwa taabu sana maana wenigine hawakuwepo hapa nchini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…