mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,420
- 17,722
Dangote anafunga kiwanda cha nyanya baada ya kukosa malighafi.
Sasa anafanya mazungumzo na kampuni ya Kiitaliano ili ije Nigeria kulima nyanya kwa wingi ili apate uhakika wa malighafi za kiwanda chake cha Tomato paste.
Kwa nini Alifungua hicho kiwanda?
Kuna kipindi hapo nyuma kama ilivyotokea hapa nchini nyanya nigeria zilikuwa nyingi kupita kiasi na bei kushuka saana. Wito ukaja watu wajitokeze kwenye kuwekeza katika usindikaji wa nyanya ili zisioze na ziuzwe mahala mbalimbali.
Dangote alipoiona hiyo fursa, iliyochochewa na wanasiasa aliamua kuwekeza kiwanda kikubwa sana cha kuchakata nyanya. Akafikilia plan B ikitokea kuna upungufu akaajiri wakulima wadogowadogo walime nyanya zisaidie.
Baada ya kiwanda kufunguliwa nyanya zilizokuwepo ziliweza kutosha kulisha kiwanda hicho kwa wiki kadhaa tu, baadae zikawa hadimu.
Wakati hayo yakiendelea, Umbali kidogo tu na nigeria Ipo nchi ya Hispania ambayo nyanya ni bei che kiasi cha kutumiwa kwenye michezo ya kupondana. Hawezi kuagiza nyanya nje ya nchi kutokana na sheria ngumu, lkn jamaa wa ndani uwezo wao ni mdogo kuzalisha kulisha nyanya kiwanda hicho jamaa amejikuta kastack inabidi atafute muwekezaji wake aje amlimie.
Chanzo:Why Dangote Closed his Tomato Factory and Lessons you can Learn from It | Opinions.ng
Najaribu kuwaza kwa nia nyororo...
1:Je hii case tumejipangaje katika kukabili changamoto zetu ili viwanda vyetu viwe endelevu?
2:Nguvu kiasi gani tumeiweka kuimarisha wakulima ili viwanda vichanue na kudumu?
3:Je, Kuna somo lolote la kujifunza au mambo yako vizuri hadi sasa?
Wataalam wa mambo karibuni katika kutoa michango nufaishi.
Mitale na midimu
Katika tafakari njema ya viwanda japo ni muumini sugu wa Kilimo na teknohama.