Kufungwa jalada la Ben Saanane jumuiya ya kimataifa yashangazwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,242
34,903
Jumuiya ya kimataifa imeshangazwa na kitendo cha ofisi ya mkugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) nchini Tanzania kufunga jalada la uchunguzi la Ndg.Ben Saanane na kukiri kwamba imeshindwa kupata taarifa za kuwezesha kupatikana kwake.

...
Ripoti ya mkutano wa kimataifa wa Haki za binadamu uliomalizika mwishoni mwa wiki (ambapo suala la Ben lilijadiliwa), inaonesha kuwa mkutano huo haukuridhishwa na namna suala la Ben lilivyohitimishwa kufuatia ofisi ya DCI kufunga jalada la uchunguzi huku kukiwa na sintofahamu juu ya kupotea kwake.

Mwezi uliopita ofisi ya DCI ilitoa taarifa kuwa imefunga rasmi jalada la uchunguzi la Ndg.Ben Saanane baada ya kukosa taarifa zozote zinazoweza kufanikisha kupatikana kwake.

Ben amepotea takribani miezi minne sasa.!

Malisa GJ
-Mwenyekiti UTG
 
Hawajamaliza tu Christmas na holiday ya mwaka mpya kama walivyoahidi ili watoe tamko leo?
 
Sasa tunawekeza nguvu zetu kwa Wema Sepetu na Daudi Bashite, hii kick lazima itatu-boost
 
Mbowe ambae ndio muajiri wa Ben amekataa kutoa ushirikiano na kuwakataza kabisa bavicha watoe hashtags za Ben halafu unakuja kutoa povu humu.
Chadema ni wasanii,mnajua ben alipo mnataka kuumiza watu vichwa tu.Mbowe anakwenda mahabusu kumuona Lema,anashindwa kwenda Moshi jirani tu kuonana na familia ya Ben.
Kiongozi wa chadema kubenea alishasema Ben anaonekana kwenye vijiwe vya kahawa,kwa hiyo msitusumbue
 
Chadema hawako serious, yaana kada wao anapotea halafu wao wala hawana effort zozote za maana za kuhakikisha anapatikana!!. Yaani kiufupi wamempotezea!. Laiti nguvu kama zilizotumika kumtetea Mbowe zingetumika kumtafuta Beni, huenda angekuwa ashapatikana!!
 
Subhana Allah, basi si watoe maelezo walivyoshindwa. Tuache siasa penye maisha ya mtanzania.

Hapa kuna wawili wanahitajikakutueleza ukweli.

1. Serakali inayo uwezo mkubwa wa kulifuatilia jambo hilo na kutufafanulia yaliyojiri mpaka kutoweka kwa mtanzania mwenzetu. Wanvyo vyombo muhimu kwa shughuli hizi.
2. Chadema nao wanao uwezo kutufafanualia mengi sana , na ukweli ukapatikana.

Kuna kitu hizi taasisi mbili zinazijua na wanatuficha , liko jambo . Cha kushangaza Chadema kama hakuna wanalolificha au kuhusika kwa vyovyote wasinge nyamaza kimya, wangelitumia hili jambo kisiasa kuikashifu serekali , mbona issue ya Wema na wengine wanayabeba kichwani, lakini hili la kada maarufu wa chadema haliwastui. Tutaona watakuja na msimo wa kupindisha ukweli .

Serakali nayo inazidi kujiingiza gizani kwa kulifunga jalada. Au sijui ndio mbinu mpya za uchunguzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…