Girland
JF-Expert Member
- Jan 24, 2016
- 2,489
- 4,240
Nimemsikiliza balozi wa Uingereza nchini Tanzania anayemaliza muda wake David Concur anasema wazalishaji wengi wa Tanzania wanashindwa kulihudumia soko la ndani kwa sababu bidhaa za kuagiza ni nafuu zaidi. Hii inasababisha viwanda vichache kufunguliwa na kupelekea upungufu wa ajira.
Mfano mzuri, ni vitenge vinavyozalishwa hapa nchini bei yake ni juu kuliko vinavyoagizwa nje hii inamaanisha gharama za uzalishaji Tanzania ni kubwa kupitiliza.
Ukienda kariakoo, na masoko yote makubwa utagundua bidhaa nyingi zinatengenezwa China. Hata vifaa Kama furniture vinatokea China ilhali mazao ya misitu yanatoka huku Africa.
Tunashindwa nini kuongeza uzalishaji? Sera mbovu!, nini kifanyike tuwajengee uwezo wazawa na wageni kuweka viwanda nchini.
TIC inajitahidi kuhamasisha uwekezaji lakini ni lazma ziwepo jitihada za makusudi kurekebisha Sera zetu. Nchini China, Taiwan, India au Korea uchumi wa viwanda unachangia Sana pato la taifa.
4R HOYEE