Siamini kabisa kwamba kuna wasomi walikaa sehemu wakajadili na kulipana posho za kikao kwamba:
Magari yanayodaiwa ushuru wa maegesho (parking) Yaanze kufungwa minyororo ili kushinikiza wamiliki kulipia tozo hizo.
Huu ni utaratibu wa hovyo sana
1. Huu utaratibu ni Hovyo kwasababu unatupunguzia wateja sisi wafanyabiashara Kariakoo, Ilala! Sisi wafanyabiashara tunalipia leseni manispaa, tunalipia zimamoto, tunalipia pesa za usafi, tunalipa kodi nyingi tu ili tufanye biashara, Mnapowafungia wateja wetu magari yao mnawatisha kwamba wasije ilala kwamba watakamatwa hili peke yake linatuondolea wateja katika biashara zetu.
2. Jambo jingine la kushangaza hivi nyie wachukua maokoto ya ushuru mmechangia nini kwenye kuwekeza maegesho hadi mchukue ushuru wa maegesho? Magari mengi yanaibiwa kwenye maegesho na ushuru wanalipa, agari yanaibiwa vipuri au taa yakiwa kwenye maegesho huo ushuru mnaolipwa je unafaida gani kwa mwenye chombo kama hamyalindi magari yao wala hamlipi fidia linapotokea janga au uharibifu?
3. Wizara na serikali kwa ujumla mlipopitisha huu utaratibu wa ushuru wa maegesho mlitegemea kwamba hawa wenye magari waendeshe halafu wakapark wapi!?
Gari ileile moja mnaitoza ushuru kibao hamuoni hiyo ni kero jaman
Huu utaratibu wa kutoza ushuru maegesho haupaswi kabisa kuwepo, ni utaratibu wa hovyo kabisa.
Mwenye gari katoka zake nyumbani kisitaarabu kufuata huduma kwa mfanya biashara halafu nyie kama serikali mnavalisha watu vibrauzi vya njano kwa kazi ya kufungia wateja wetu magari yao mnataka wateja tupate wapi wakiogopa kuja mijini?
Kwanini mnapenda kuifanya nchi yetu sote iwe kero kwa wengine jamani.

- gari ileile mnaitoza ushuru wa kuingiza nchini (TRA)
- Mnaitoza Ushuru wa kutumia barabara (road licence) kwenye kila lita moja ya mafuta mnafyeka sasa mnategemea huyu mtu akapaki porini?
- Mnamchukua nenda kwa usalama
- kwenye bima cha kwenu pia kipo na mengine mengi.