Kufuatia kifo cha Rais Magufuli, Bendera ya UN itapepea Nusu Mlingoti siku ya Mazishi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,106
10,173
Umoja wa Mataifa umetangaza kupeperusha bendera yake nusu mlingoti siku ambayo atazikwa Rais Magufuli

Rais Magufuli anatarajia kuzikwa Tarehe 26/03/2021

1616444387594.png
 
Bendera ya umoja wa mataifa United Nations(UN) itapepea nusu mlingoti Siku ya tarehe 26 March, 2021 katika makao makuu yake jijini Newyork, Marekani ambayo ndiyo siku ya kuzikwa hayati Dr Magufuli.

Pia UN imehamasisha siku hiyo bendera zote za UN katika mataifa mbalimbali kupepea nusu mlingoti.
 
HUU UTARATIBU NI WA KAWAIDA AU UMEANZA KWA HAYATI MAGUFURI??
MAANA ZITAANZA DRAMA ZA AJABU MUDA SIO MREFU
Hata kama ni utaratibu wa kawaida nafikiri ingepasa bendera hiyo isipepee kabisa nusu mlingoti maana Nchi mwanachama Rais wake miaka 6 hakuhudhuria hata Mkutano mmoja wa UN eti kwa ya kutojua Kingereza, Kisukuma nacho je?

Rais mpya anajua faida ya kuwa na Makamu anayejua lugha za Kimataifa maana yeye akiwa Makamu alimuwakilisha Rais mara kadhaa kwa hiyo asikubali CCM wamletee Rais ajaye mbumbumbu aaibishe Nchi yetu. Miaka 6 imeaibishwa vya kutosha!
 
Hawa mabeberu watakuwa wanafurahi kifo cha kiboko yao.

Sasa wanahema,maana walibananika kila kona.

Watuache tumalizane wenyewe,huo unafika ubaki kwao.

Au sio MATAGA wenzangu.
 
Wabongo wengi kwanza ni wavivu wa Kusoma, hilo halina ubishi, hivyo kwa sababu inajulikana hii huwa kuna watu wanaitumia kwa manufaa yao wenyewe.

Anapo kufa Kiongozi wa Nchi Mwanachama wa UN bendera ya UN hupepea nusu mlingoti kwenye jengo lake la makao mkuu pale New York.

Hii ni sheria sio utashi wa Katibu mkuu wala nini.

Hivyo kwa sababu Mheshimiwa Hayati Magufuri alikuwa Raisi wa nchi Mwanachama Sheria inataka Bendera ipepee nusu mlingoti pale UN.
 
Back
Top Bottom