Kuflash simu bila kutumia dongle/box

yutu

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
1,633
973
Habari zenu wakuu?
Kadiri siku zinavyokwenda na teknolojia nayo inakuwa kwa kasi kubwa sana so nimeona nitumie uwanja huu kupata na kujuzwa kwa kina kidogo kwa hili linalonitatiza
nalo kabla nilikuwa Nina mpango wa kununua box la kuflashia simu aina ya milacle lakini katika kufatilia nikakutana na mtaalamu maeneo ya Kariakoo akaniambia kwamba anaweza kuniuzia software proglam ambayo ina uwezo wa kuflash simu bila matatizo kwa gharama ya laki na nusu tu na yuko tayari kunitestia na kuiona jinsi inavyofanya kazi.

Hivyo naomba mawazo yenu kama huu utaalamu unawezekana na kama unawezekana faida na hasara zake ni zipi tofauti kama ntakuwa na box.

Asanteni
 
angalia asikuingize mjini software zipo ila ninavyofahamu mimi hakuna software inayoflash simu zote au kutatua matatizo ya simu zote, zipo zinazoflash mediatek, samsung, nokia nk

pia unaponunua box unapata support toka kwa watengenezaji incase umekwama au kuna tatizo jipya.

na software nyingi za kuflash simu ni bure hio ya laki na nusu ndio ipi? muulize jina halafu ilete hapa tuhakikishe kama kweli ina thamani hio.

pia kumbuka box pia hutumika ku unlock simu, ikiwa utatarget simu za bongo zinazotoka sana kama huawei za tigo, modem nk unarudisha hela ya box muda mfupi tu, ila itabidi ukae chini ufanye research ya box zuri kwa mazingira yetu
 
Ningekushauri tengeneza ujamaa ujamaa na mafundi simu kwanza hizo software ni free online
Au mfate hamza ma iPhone akufundishe kwa low price pale mobile plaza
 
Software za kuflash simu ni free tu online tena ni rahisi kuzitumia..iyo laki labda akuuzie box
 
Sp Flashtool = all MTK devices (All tecno) files on Hovatek.com

Research Download = All spreadtrum devices (Itel) files on HOvatek.com

Odin=All samsung devices Files on sammobile.com

Huawei=files on huawei website

Sony=Flashtool files on sony website

iPhones/iPads/iPods = itunes

yaani smartfone karibu zote hakuna haja ya kua na box, just internet
 
Mkuu nauliza ivii.... Izo software unaweza unlock cellphone kama Nokia torch ivii au izi simu za voda za promotion?
 
Dad's chief damaging bilious naomba kujua kuhusu Samsung galaxy note edge husudani ubora wake
 
mkuu hapo ktk Huawei.
Nimeingia website yao lakini
sikupata msaada wowote.
Nilikuwa nataka kujua namna ya kuflash
Huawei na kupata firmware. Nimeshindwa kujua
Huawei inatumia software gani kuflash kama ulivyoweka
kwa Samsung odin, na hizo zingine.
Maelekezo zaidi mkuu
 
huawei unaeka firmware kwenye memory card.
1. download firmware
2. extract hio firmware utapata file la update.app
3. eka memory card kwenye simu
4. tengeneza folder linaloitwa dload
5. eka file lako la update ndani ya folder la dload

ukimaliza hizo step zima simu then bonyeza volume up, volume down na power key kwa pamoja ku update

au nenda setting halafu about halafu update halafu local update.
 
Ahsante Chief-Mkwawa kwa maelezo mazuri.
Samahani kuweza kupata firmware za Huawei.
Manake naona kuna site tofauti tofauti sasa sijui
ipi ni Official
 
Ahsante Chief-Mkwawa kwa maelezo mazuri.
Samahani kuweza kupata firmware za Huawei.
Manake naona kuna site tofauti tofauti sasa sijui
ipi ni Official
official ni website yao wenyewe huawei angalia domain ukiona imeandikwa huawei.com jua hapo ndio mahali salama pa kudownloadia.

mfano simu inaitwa y530 andika google

huawei y530 firmware

utaona result ya kwanza kabisa inatoka website inaitwa consumer.huawei.com then hio ndio official
 
Ahsante nimejaribu kugoogle
zimekuja website nyingi lakini sijaona
iliyoandikwa huawei.com
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…